Faisans: Kisiwa cha kinachobadili utaifa kila baada ya miezi sita

kisiwa cha Faisans kinachomilikiwa na Ufaransa na Uhispania kwa awamu Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Utaratibu wa makabidhiano ya umiliki wa kisiwa cha Faisans ni utaratibu ambao umekuwepo kwa zaidi ya miaka 350

Wiki ijayo, Ufaransa itakabidhi kisiwa cha kilomita mraba zaidi ya 3,000 kwa Uhispania bila risasi hata moja kufyatuliwa.

Lakini katika muda wa miezi sita Uhispania itarejesha tena ardhi hiyo kwa hiari kwa Ufaransa.

Huu ni utaratibu ambao umekuwepo kwa zaidi ya miaka 350.

Mji wa Hendaye katika ufukwe wa mwambo wa Ufaransa wa Basque kimsingi ndio mji wa mwisho kabla ya kufikia kwenye mwisho wa mpaka Uhispania.

Kwa mbali utadhani ni eneo zuri lililozingirwa na rundo la mchanga ambalo linaonekana kukaliwa na mamia ya wanyama wa majini.

Lakini ukitazama kwa karibu utabaini ukweli kwamba si wanyama bali ni wachezaji wa michezo ya kuteleza kwenye barafu ambao wamevalia mavazi yaliyolowa maji.

Nyuma kidogo ya kingo za maji upo mji wa kihistoria wa Uhispania wa Hondarribia na majengo yake yamesambaa, na kupakana na mji jirani wa Irun.

Mpaka asilia kati ya Uhispania na Ufaransa ni mto Bidassoa, unaomwaga maji yake kwenye mlango wa mto ambao umetenganisha nchi hizo mbili.

Image caption Kisiwa cha Faisans ni kidogo sana - kina urefu wa mita 200 pekee na upana wa mita 40

Kadri unavyopanda kutoka kwenye mwisho wa mto, taswira hubadilika. Unapita majengo ya rangi za kuvutia ya mji wa Basque na kuanza kuyaona majengo ya maghala ya viwanda upande wa Ufaransa, upande ule mwingine ukiyaona majengo yasiyo ya kuvutia ya wakazi upande wa Uhispania.

Lakini kile kinachowavutia wengi eneo hilo ni kisiwa cha Faisans. Si rahisi kukipata. Unapoomba kuelekezwa hakuna mtu anayeelewa ni kwa nini unataka kwenda pale.

Watakwambia hakuna kitu cha kuangalia na unaonywa kuwa huwezi kukitembelea kisiwa hicho na kwamba hakuna yeyote anayeishi huko, si mahala pa utalii kama Mont St Michel.

Lakini hapo ndipo kilipo kisiwa cha amani, kisichoweza kufikika kati kati ya mto, chenye miti na nyasi zilizokatwa vizuri, pamoja na mnara wa zamani ambao ni ishara ya tukio kubwa la kihistoria lililotokea mwaka 1659.

Kwa miezi mitatu, nchi za Uhispania na Ufaransa zilikubaliana kumaliza vita vya muda mrefu vya mataifa hayo kwenye kisiwa hiki, kwa sababu kilikuwa kinaangaliwa kama eneo huru.

Madaraja ya mbao yalipanuliwa kutoka pande zote. Majeshi yalisimama tayari pale mazungumzo yalipoanza.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mfalme Louis XIV wa Ufaransa na Philip wa IV wa Uhispania walipokutana kwenye kisiwa cha Faisans mnamo mwaka 1660

Mkataba wa amani unaofahamika kama - Mkataba wa Pyrenees - ulitiwa saini hapo.

Eneo lilijadiliwa na mpaka ukachorwa. Na mkataba ukakamilishwa kwa harusi ya kifalme, pale Mfalme wa Ufaransa Louis XIV alipomuoa binti wa mfalme wa Uhispania Philippe IV.

Moja ya mambo yaliyoafikiwa kwenye mkataba huo ni kwamba kisiwa chenyewe kingekuwa kisiwa cha nchi mbili, udhibiti wake ukiwa wa awamu kutoka nchi moja kuelekea nyingine.

Kwa miezi sita ya mwaka, kuanzia Februari hadi Julai kitakuwa chini ya utawala wa Uhispania - na kwa miezi sita inayofuatia kinakuwa mali ya Ufaransa.

Aina hii ya umiliki wa pamoja wa eneo hujulikana kama 'condominium' - ile hali ya mataifa mawili kudhibiti eneo kwa pamoja - , na kisiwa cha Faisans ni moja ya maeneo ya kale zaidi yanayotawaliwa kwa mtindo huu.

Kisiwa hiki ni kidogo sana - kikiwa na urefu wa mita 200 pekee na upana wa mita 40.

Ni nadra sana kwa watu wa kawaida kutembelea kisiwa hiki katika siku za maadhimisho ya turathi, lakini kulingana na afisa anayehusika na utunzaji wa kisiwa hizo Benoit Ugartemendia wazee na vijana hawatambui lolote kuhusu umuhimu wake wa kihistoria.

Siku hizi, mameya wa Irun na Hendaye hukutana mara nyingi kwa mwaka kwenye kisiwa hiki kujadili masuala kama ya maji safi na haki za uvuvi.

Miaka ya nyuma wavuvi wa Kihispania walilalamika kuhusu muundo wa maboti ya Ufaransa na hivi karibuni wamekuwa wakikerwa na boti za Wafaransa wanaotembelea kisiwa hicho kwa mapumziko ambao wanasema wanavuruga biashara zao.

Kisiwa chenyewe hakipewi kipaumbele sana.

Udongo wake unamomonyoka - kimepoteza karibu nusu ya ukubwa wake kwa karne kadhaa, kwa sababu theluji inayoyeyuka kutoka kwenye milima na kuingia ndani ya mto. Lakini hakuna nchi inayotaka kutumia pesa zake kujenga ukingo wa kisiwa hiki.

Mwaka huu, hakutakuwa na sherehe ya makabidhiano ya kisiwa hiki.

Kulikuwa na wazo la kupeperusha bendera ya nchi yoyote ambayo inakimiliki - lakini Meya wa upande wa Uhispania Ecenarro anasema kuwa hilo lingewachochea wanaotaka kujitenga kwa Basque kuishusha ama kuweka bendera yao.

Kwa hivyo katika muda wa siku chache - labda mpaka huu ambao hauzozaniwi zaidi duniani utabadili mmiliki wake tena.

Na mwezi Agosti Uhispania itarejesha umiliki wa kisiwa hiki tena labda isipokuwa tu pale itakapoamua kuvunja utaratibu huu uliodumu kwa zaidi ya miaka 350.

Mada zinazohusiana