Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 29.01.2018

Joe hart Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mlinda lango Joe Hart yuko makini kumalizia mkataba wake wa deni na West Ham kabla ya msimu wa kuhama kumalizika

Mshambuliaji wa Manchester United striker Zlatan Ibrahimovic anakaribia kabisa kuhamia LA Galaxy katika MLS. Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 36 mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Sweden anakaribia kurejea katika mazoezi wiki ijayo baada ya kupata jeraha mwezi Disemba (ESPN).

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasisitiza kuwa anahitaji washambuliaji watatu katika kikosi chake ili kuweza kuwa na uwezekano wa kushinda taji msimu huu. (Express).

Mlinda lango Joe Hart yuko makini kumalizia mkataba wake wa deni na West Ham kabla ya kipindi cha kuhama kumalizika. Hart mwenye umri wa miaka 30 wenye deni la Manchester City, kwa sasa ni chaguo la pili la David Moyes na anataka kusalia na nafasi yake kama mchezaji nambari moja wa England katika Kombe la Dunia (Times )

Andre Ayew anaweza pia njiani kuelekea West Ham huku Swansea ikitumai kumaliza mkataba wa Euro milioni 18m kwa ajili ya kurejea kwa mchezaji huyo raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 28 katika Liberty. (Sun)

Manchester United imeingia katika mbio za kusaini mkataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Bayern Munich kutoka Chile Arturo Vidal, mwenye umri wa miaka 30. (Mirror)

Mshambuliaji wa West Ham na Senegal Diafra Sakho, 28, amefufua mazungumzo na klabu ya Rennes kuhusu uwezekano wake kuhamia klabu hiyo ya Ufaransa kwa £9m. (Mail)

Image caption Manchester United imeingia katika mbio za kusaini mkataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Bayern Munich kutoka Chile Arturo Vida

Nyota wa Brazil anayechezea Monaco Fabinho, 24, ambaye amehusishwa na kuhamia Manchester United au Manchester City, ameashiria kwamba anataka kuihama klabu hiyo ya Ufaransa kutafuta changamoto mpya. (Lancenet kupitia Sky Sports)

Mazungumzo ya mshambuliaji wa Roma Edin Dzeko, 31, kutoka Bosnia kuhamia klabu ya Chelsea yamesambaratika. (Star)

Meneja wa Watford Javi Garcia atajaribu kumfanya kiungo wa kati wa Sunderland na Gabon Didier Ndong, 23, kuwa mchezaji wake wa kwanza kumnunua tangu apewe kazi hiyo. (Sun)

Image caption Jose Mourinho amehakikisha kabati la mchezaji wake mpya Alexis Sanchez linakaribiana na la Marcus Rashford kuhakikisha uhusiano kati ya wawili hao unaimarika

West Brom wako tayari kuwasilisha ofa ya £18m kutaka kumnunua mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 29. Mwingereza huyo hakuchezea klabu hiyo ilipolazwa Kombe la FA Jumamosi. (Birmingham Mail)

Newcastle huenda wakarejea na ofa ya tatu na ya mwisho kwa mshambuliaji wa Feyenoord na Denmark Nicolai Jorgensen, 27, katika saa 24 zijazo. (Chronicle)

Crystal Palace wanatafakari uwezekano wa kuwasilisha ombi la kumtaka mshambuliaji Mwingereza wa Burnley Ashley Barnes, 28, ambaye amesalia na miezi 18 pekee katika mkataba wake wa sasa Turf Moor. (Sky Sports)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amehakikisha kabati la mchezaji wake mpya Alexis Sanchez linakaribiana na la Marcus Rashford kuhakikisha uhusiano kati ya wawili hao unaimarika ndani na nje ya uwanja. (Sun)

Klabu ya Ujerumani ya FC Kaiserslautern ndiyo ya karibuni zaidi kumtaka mshambuliaji kutoka Sweden anayechezea Bristol City Gustav Engvall, 21. (Sport Bladet kupitia Bristol Post)

Image caption Meneja wa Blues Antonio Conte anasisitiza kuwa mshambuliaji mbelgiji Michy Batshuayi sio lazima Blues mwezi huu

Stoke City itatakiwa kulipa Euro milioni 16 kugharimia usajili wa mchezaji wa Galatasaray na mchezaji wa kiungo cha kati kutoka Senegal Badou Ndiaye. Stoke City tayari walikataliwa mkataba huo kwa Euro milioni 14 kwa ajili ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 27. (Sun)

Arsenal watamruhusu mchezaji fowadi Olivier Giroud kuhamia Chelsea ikiwa mahasimu wao katika Premier League watakubali kumgharimia Mfaransa huyo mwenye 31 kwa Euro milioni 35 anazozitaka. (Mail)

Meneja wa Blues Antonio Conte anasisitiza kuwa mshambuliaji mbelgiji Michy Batshuayi mwenye umri wa miaka 24 ambaye anahusishwa na deni la kumuondosha kwenye kilabu chake, sio lazima aondoke mwezi huu. (Evening Standard).

Mshambuliaji wa West Ham na Senegal Diafra Sakho, 28, amefufua mazungumzo na klabu ya Rennes kuhusu uwezekano wake kuhamia klabu hiyo ya Ufaransa kwa £9m. (Mail)

Kutoka Jumapili

Manchester City wako tayari kuwasilisha £150m kumtaka nyota wa Chelsea Eden Hazard, 27, baada ya Pep Guardiola kumtambua winga huyo wa Ubelgiji kama mchezaji anayetaka kumnunua zaidi majira yajayo ya joto. (Sunday Mirror)

Arsenal watahitajika kuwalipa Borussia Dortmund £60m kumchukua Pierre-Emerick Aubameyang, 28, la sivyo walazimike kumtafuta mshambuliaji mwingine. (Sunday Mirror)

Mwenyekiti wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi amepuuzilia mbali tetesi kwamba Neymar, 25, anaweza kuhamia Real Madrid na kusisitiza kwamba ana uhakika "2,000%" kwamba mchezaji huyo atakuwa katika klabu hiyo ya Ligue 1 msimu ujao. (Mail on Sunday)

Manchester City na Manchester United wanashindana kumtaka kiungo wa kati wa Brazil Fred, 24, kutoka Shakhtar Donetsk. (Daily Star Sunday)

Liverpool na Tottenham nao wanaonekana kuambulia patupu katika kumtafuta kiungo wa kati wa Paris St-Germain Javier Pastore, 28, ambaye amethibitisha kwamba anataka zaidi kurejea Italia. (Metro)

Mada zinazohusiana