China yakanusha upelelezi dhidi ya AU

Jengo la Umoja wa Afrika Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jengo la Umoja wa Afrika

Serikali ya China imekanusha kuwa ripoti iliyotelewa na gazeti binafsi la Ufaransa la Le Monde kuwa imekuwa ikifanya upelelezi dhidi ya makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) yaliopo jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Taarifa hiyo ilidai kuwa kwa muda wa miaka 5, habari kutoka jengo la AU, lililojengwa na Wachina, zilikuwa zikipelekwa jijini Shanghai usiku wa manane.

Balozi wa China katika Umoja wa Afrika, Kuang Weili, alitaja ripoti hio kuwa "isiyo na mantiki" na "ya kupotosha."

Pia alitia shaka kwenye siku ripoti hio ilitolewa, ambapo ilitolewa siku moja kabla ya viongozi wa Afrika kuanza mkutano wao wa mwaka katika makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Jengo hilo lenye gorofa 20 liligharimu dola za Marekani milioni 200 na limekuwa makazi ya bodi hiyo ya Bara la Afrika tangu mwaka 2012.

Mada zinazohusiana