Uchambuzi: Udhaifu wa huduma ya dharura ya moto Kenya

A resident reacts after running out of water as they attempt to extinguish a fire that broke out at the Kijiji slum in Southlands estate of Nairobi, Kenya January 28, 2018 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanaume mmoja akijaribu kukimbia baada ya maji kumuishia akizima moto eneo la Kijiji

Picha ya Rais Uhuru Kenyatta akitabasamu, wakati akijaribu mpira wa gari jipya la kuzimia moto akiongozana na gavana wa Nairobi Mike Sonko Mbuvi , ilianza kusambaa tena mitandaoni baada ya nchi hiyo kujikuta tena katika janga la moto.

Taifa hilo bado limeshindwa kukabiliana vilivyo na mikasa ya moto.

Gavana Mbuvi aliweka picha hiyo kwenye mtandao wa Twitter mwaka jana mwezi wa kumi aliposema kwamba amepata magari mapya 24 ya kuzimia moto na kwamba magari hayo yangekuwa msaada mkubwa kuyakabili majanga ya moto ambayo yamekuwa yakiwakabili mara kwa mara.

Miezi mitatu baadaye, janga la kwanza la moto linaibuka na kugeuka kipimo kwa jeshi la zima moto na idara hii muhimu inashindwa kukabiliana na jaribio hilo.

Eneo lijilikanalo kama Kijiji, umbali wa takribani kilomita 10 tokea katikati ya mji wa Nairobi, lilishika moto majira ya saa mbili za usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki na ulipozimwa kabisa masaa kumi baadaye watu watatu tayari walikuwa wamepoteza maisha sababu ya moto huo na eneo hilo lote lisilo rasmi kwa makazi lilikuwa limeteketea kwa moto

Wengi wanajiuliza kwa nini kikosi cha zima moto kimeshindwa kwa kiwango cha juu kuukabili moto huu licha ya kuwa na vifaa vipya?

Si mara ya kwanza magari ya zima moto yanaishiwa maji wakati yakizima moto, na yanapotaka kujazwa tena maji lazima yasafiri umbali mrefu, si chini ya kilomita 20 mpaka mjini kati , Piusi Maasai mwenyekiti wa tume ya kukabiliana maafa anasema eneo hilo halikuwa na maeneo maalumu kwa ajili ya magari hayo kujazia maji.

Haki miliki ya picha Reuters

Ni magari manne pekee ya zima moto, yalitolewa ikiwa ni idadi ndogo kabisa kwa janga hilo kubwa ambalo limeziacha karibu kaya 6000 bila ya makazi na swali litaendelea kusalia. Kwanini mamlaka haziku ruhusu magari zaidi kwenda eneo la tukio? Bwana Maasai alirekodiwa akiomba magari zaidi

Jeshi halikusaidia chochote licha ya kambi yake ya Langata kuwa umbali wa kilomita moja toka eneo la tukio. Jeshi la Kenya huwasaidia wananchi wakati wa majanga mpaka sasa haiku wazi kwa nini hawakutoa msaada mara hii wakati moto walikuwa wanauona.

Makazi yasiyo rasmi kama Kijiji yanakuwa hayana mpangilio mzuri, nyumba husongamana sana na hakuna njia za katikati, hivyo magari yazima moto yasingeweza kuingia ndani zaidi na ndiyo sababu yakalazimika kusalia kwenye barabara za nje kuzunguka makazi hayo.

Mara zote swala hili limekuwa likiibuliwa pindi majanga ya moto yanapotokea na maafisa mipango miji hawajawahi kuchukua hatua madhubuti baada ya majanga licha ya kauli hii kutolewa mara kwa mara.

Haki miliki ya picha Reuters

Jeshi la polisi linapeleleza kujua chanzo cha moto huo lakini Wakenya wameghadhabishwa kwamba kwa mara nyingine janga limetokea na wenye wajibu wa kupambana nalo wameshindwa.

aadhi wamefikia hatua ya kusema wakati wa uchaguzi magari ya polisi hayakuishiwa maji ya kuwasha kupambana na waandamanaji.

Gavana wa Nairobi ana maswali mengi ya kujibu, hajazungumza bado.

Mada zinazohusiana