Mkurugenzi wa CIA anasema Urusi itaingilia uchaguzi wa katikati ya muhula

Trump na Putin Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Donald Trump amekuwa akishukiwa kutokana na uhusiano wake na rais wa Urusi Vladimir Putin

Mkurugenzi wa wataalam wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, anatarajia kuwa Urusi itailenga Marekani katika uchaguzi wa kati kati ya muhula baadae mwaka huu.

Mike Pompeo ameiambia BBC kuwa hakujawa na ushahidi wa kutosha wa kuonyesha kuwa Urusi haikufanya majaribio ya kuziangusha tawala Ulaya na Marekani.

Pia amesema kuwa Korea Kaskazini inaweza kuwa na uwezo wa kuishambulia Marekani kwa makombora ya nuklia "katika kipindi cha miezi michache".

Idara za ujasusi za Marekani zimesema kuwa zinaamini kwamba Urusi iliingilia katika uchaguzi wa mwaka 2016 .

Hivi karibuni Bwana Pompeo alidai kuwa rais wa Marekani Donald Trump hayuko tayari kutekeleza majukumu yake.

Chumba cha mkutano wa wakurugenzi kilichopo kwenye ghorofa ya saba ya makao makuu ya CIA eneo la Langley, Virginia, kina msururu wa picha za wakurugenzi wa zamani wa CIA na marais waliowahudumia.

Bwana Pompeo ni mwazi juu ya malengo yake kwa CIA chini ya utawala wa rais Trump.

Image caption Bwana Pompeo anasema kuwa bado anaiona Urusi kama adui

"Tutakwenda nje na kuiba siri kwa niaba ya watu wa Marekani. Na nilitaka tufanye kazi kwa bidii."

Baada ya mwaka mmoja mamlakani, Bwana Pompeo anasema jukumu lake limekuwa ni la kulipunguzia matatizo shirika la CIA.

Ni shirika linalofanya kazi katika dunia ambayo haitabiriki, dunia ambayo tathmini ya ujasusi inaweza kuwa kwa misingi ambayo si ya hatua za kijeshi, bali pia utata wa kisiasa.

Licha ya kwamba kumekuwa na ushirikiano katika kukabiliana na ugaidi, Bwana Pompeo anasema kuwa bado anaiona Urusi kama adui, hofu ambayo nchi za Ulaya zinayo .

"Sijaona ushahidi wa kuridhisha wa kupungua kwa shughuli zao" alisema.

Alipoulizwa ikiwa hofu zake zinahusiana na uchaguzi ujao wa kati kati ya muhula wa mwezi Novemba, alijibu, "Bila shaka. Nina matarajio kwamba wataendelea kujaribu kufanya hivyo, lakini ninaamini kwamba Marekani itakuwa na uwezo wa kufanya uchaguzi ulio huru na wa haki kiasi kwamba athari zao kwenye uchaguzi huo hazitakuwa kubwa.

Bwana Pompeo anasema Marekani inajishughulisha katika kujaribu kukabiliana na njama za Urusi. Baadhi ya kazi hizi hazikuwa jukumu la CIA, kama vile kuwasaidia watu kuthibitisha uhakika wa vyanzo vya taarifa.

Image caption Bwana Pompio anasema baadhi ya kazi wanazozifanya hazikuwa jukumu la CIA kama vile kuwasaidia watu kuthibitisha uhakika wa vyanzo vya taarifa.

Lakini taasisi za ujasusi zilihusika katika utambuzi wa nani alikuwa nyuma ya njama za uadui, kwa kutumia mbinu za kiufundi kuzizuia na kujaribu kuizuia Urusi kutekeleza njama hizo.

Bwana Trump amekuwa mtu wa kupinga madai ya uingiliaji wa Urusi kinyume kabisa na matokeo ya uchunguzi wa taasisi za ujasusi za Marekani. Je, Mkurugenzi mkuu amechukua mwelekeo ulio sawa?

"Sifanyi yaliyo sawa. Ninatekeleza ukweli," alijibu. "Tunawajibika walau kila siku, kwa rais kuelezea ukweli tunaoufahamu kutoka CIA."

Bwana Pompeo humpa taarifa Bwana Trump karibu kila mara wote wanapokuwa mjini Washington DC. Taarifa hizo zinahusu matukio ya karibuni na masuala ya mikakati.

Mada zinazohusiana