Wachezaji wawili wanaomzuia Aubameyang kutua Arsenal kwa sasa

Aubameyang
Image caption Arsenal wanamtafuta Aubameyang kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez ambaye alijiunga na Manchester United mapema mwezi huu

Kufanikiwa kwa Arsenal kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang kwa £60m kutategemea makubaliano kuhusu wachezaji wengine wawili.

Na mshambuliaji wa Gunners Olivier Giroud ndiye huenda akawa na usemi zaidi kuhusu iwapo mkataba wa kuhama kwa Aubameyang utakamilishwa kabla ya muda wa mwisho wa kuhama wachezaji kipindi hiki, Jumatano saa 23:00 GMT.

Arsenal wamekubali kulipia gharama na mikataba ya kibinafsi ya mchezaji huyo kutoka Gabon mwenye umri wa miaka 28.

Lakini Dortmund itaidhinisha hatua hiyo kama watapata mchezaji wa kuchukua nafasi yake.

Mchezaji soka wa kimataifa wa Ufaransa Giroud, mwenye umri wa miaka 31, aliorodheshwa kuwa ndiye mchezaji atakayechukua nafasi hiyo, lakini binafsi angependelea kubaki London.

Hatua ya Chelsea kuanza kumtafuta ilimpatia nafasi hiyo ya kusalia London muda unaomfaa - na hivyo basi Dortmund wameelekeza matumaini yao kwa mshambuliaji wa Chelsea Mbelgiji Michy Batshuayi, ambaye anaweza kuwa tayari kuhama.

Batshuayi akahamia Dortmund basi Chelsea wanaweza kufanikiwa kumchukua Giroud.

Batshuayi, mwenye umri wa miaka 24, amekuwa akichezeshwa sana kama mchezaji wa kuongeza nguvu mpya katika kikosi cha Chelsea na anataka kucheza zaidi kikosi cha kwanza katika mwaka wa Kombe la Dunia.

Hata hivyo, the Blues wanasita kukubali bei ya Arsenal ya kumnunua Giroud ambayo iliripotiwa kuwa ni kati ya £30m-£35m.

Image caption Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hataki kumwacha Olivier Giroud aondoke Emirates

Matokeo yake Chelsea ilifanya mazungumzo na Tottenham Hotspur ikitaka imchukue Batshuayi na kuipatia Chelsea mmshambuliaji wake Fernando Llorente raia wa Uhispania mwenye umri wa miaka 32.

Spurs wako makini kuingia mkataba wa kudumu, ingawa Chelsea inapendelea uhamisho wa mkopo

Bado hilo limetatizwa na haja ya Batshuayi kuwa katika timu ya kwanza ya soka.

Hii ni kwa sababu ana nafasi ndogo sana yake yeye kumuondoa mshambuliaji mkuu wa Spurs Harry Kane - ambaye ndiye mchezaji mwenye magoli mengi.

Batshuayi hataki kuwa mshambuliaji wa akiba katika klabu nyingine.

Kama Arsenal haitaweza kufikia mkataba na Chelsea kumhusu Giroud, hatua ya Aubameyang itategemea kama Dortmund watapata mchezaji mwingine mbadala kwingine.

Kama hapatapatikana mtu wa kuchukua nafasi yake, atabakia Dortmund - kama klabu hiyo ya Ujerumani ilivyoelezea.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anampenda Giroud, lakini Mfaransa huyo amekwishaambiwa kuwa hatapata muda wa mchezo katika uwanja wa Emirates na anajua anahitaji kuwa anacheza ikiwa anataka kushiriki katika Kombe la Dunia.

Arsenal wanamtafuta Aubameyang kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez ambaye alijiunga na Manchester United mapema mwezi huu, kwa kubadilishana na kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan.

Mada zinazohusiana