Washona kutoka Zimbabwe waliokwama Kenya miaka hamsini

Washona kutoka Zimbabwe waliokwama Kenya miaka hamsini

Kwa zaidi ya miongo mitano watu 4,000 wa jamii ya Shona kutoka Zimbabwe wameishi nchini Kenya bila utambulisho wowote.

Wazazi wao walifika Kenya miaka ya sitini kuhubiri injili lakini hawakupata vitambulisho vyovyote.

Sasa Zimbabwe pia haiwatambui kama raia wake.

Mercy Juma anaelezea changamoto wanayopitia jamii hiyo.