Tana: Ziwa kubwa zaidi Ethiopia hatarini

Tana: Ziwa kubwa zaidi Ethiopia hatarini

Ziwa kubwa nchini Ethiopia, ziwa Tana linabeba nusu ya maji safi yatumikayo nchini humo, na ndicho chanzo cha mto Nile.

Ingawa juu ya mto huo kwa sasa umetanda utando wa kijani kutokana na kuvamiwa na magugu maji.

Magugu maji hayo yanawaogofya wakulima na wavuvi wanaolitegemea ziwa hilo. Watu waishio karibu na ziwa wameungana kujaribu kuondoa magugu hayo lakini kutokana na kasi ya kuenea kwake, wanahitaji suluhu nyingine.