Udhalilishaji watoto warindima Chile

Chile
Image caption Kiongozi wa Kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis

Askofu mmoja raia wa Chile ambaye amekuwa akishutumiwa kwa kuficha ukweli wa unyanyasaji wa kijinsia aliofanyiwa mtoto na padri mmoja, hatimaye ameupokea uamuzi wa baba mtakatifu kutuma mjumbe kuchunguza mashtaka dhidi yake.

Askofu Juan Barros ameeleza matumaini yake kuwa mchakato wa uchunguzi huo utatoa mwanya wa "ukweli kufichuliwa "

Askofu huyo wa visiwa vya Malta (Charles Scicluna) atakwenda nchini Chile kusikia kutoka kwa waathirika wa unyanyasaji huo.Papa ameamua akiamini kuwa kuna ushahidi mpya.

Papa Francis alikanusha hadharani madai hayo juu ya safari yake ya hivi karibuni ya Chile, lakini baadaye aliomba radhi kutokana na matamshi yake ya ukali , ingawa alijitetea kuwa si kwa ajili ya kujihami dhiti ya Askofu.