Mapigano makali yawalazimisha wengi kutoroka makwao Syria

Displaced Syrians who fled the town of Jandaris arrive in the city of Afrin (25 January 2018) Haki miliki ya picha AFP
Image caption UN inakadiria kwamba watu 5,000 wametoroka makwao tangu kuanza kwa mashambulio ya Uturuki

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya robo ya milioni ya Wasyria wamekimbilkia Kaskazini Magharibi mwa nchi tangu katikati ya Desemba, baada ya serikali kuanzisha mashambulizi makali.

Afisa wa Misaada wa Umoja wa Mataifa Ursula Mueller ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mashambulizi ya anga na mapigano katika jimbo la Idlib na kaskazini Hama yamesababisha kukimbia kwa jumla ya watu Mia mbili na sabini elfu.

Ameonya kuwa nyingi ya familia hizi wamekuwa wakiishi katika miezi ya baridi na yenye majimaji.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wengi wa Kikurdi wameuawa

Afisa huyo wa Misada wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuwa huduma za misaada katika maeneo yenye mizozo, zimekuwa zikikwamishwa na Mamlaka za chini katika maeneo mengine ya nchi.

Mada zinazohusiana