Mwezi Mkubwa wa Buluu: Kwa nini Mwezi leo unaonekana ukiwa tofauti

Wakati wa mwezi kupatwa, Mwezi huonekana ukiwa na rangi nyekundu Haki miliki ya picha SPL
Image caption Wakati wa mwezi kupatwa, Mwezi huonekana ukiwa na rangi nyekundu

Wanaopenda kutazama angani leo tarehe 31 Januari wamekuwa wakishuhudia tukio ambalo si la kawaida, Mwezi mkubwa wa kuangaza, ambao huitwa kwa Kiingereza "Super blue blood moon" (Mwezi Mkubwa wa Buluu na Damu).

Nchini Australia, Asia na maeneo ya Marekani na mashariki mwa Ulaya, mwezi unapatwa, Dunia itakapopita katikati ya Jua na Mwezi.

Usiku huu pia, Mwezi utakaribia kabisa Dunia katika njia yake ya kuizunguka Dunia.

Itakuwa pia mara ya pili kwa Mwezi kuandama katika mwezi, tukio ambalo huitwa kwa Kiingereza 'blue moon'.

Tukio kama hili lilitokea mara ya mwisho miaka 150 iliyopita, Machi 31, 1866.

Si ajabu kwamba tukio la adimu kwa Kiingereza hudaiwa kutokea 'once in a blue moon' (mara moja katika Mwezi wa buluu).

Neno "damu" hutumiwa kueleza rangi nyekundu iliyokolea inayotokea miali ya jua inapopita katika anga ya Dunia na kuangaza kwenye Mwezi.

Rangi hiyo hutokana na tukio ambalo pia hufanya anga kubadilisha rangi wakati wa kutua kwa jua, au anga mchana kusipokuwa na mawingu au vumbi kuonekana ya rangi ya samawati, anasema Dkt Shannon Schmoll, kutoka Michigan.

"Baadhi ya miali hupitia anga ya Dunia na kufika Mwezini, na pia hujipinda kiasi na kuelekea kwenye Mwezi kidogo," anasema.

Hili huondoa kiasi miali ya buluu na kuacha miali ya rangi nyekundu ikionekana zaidi.

"Na kisha, miali hiyo hujipinda kidogo kuelekea kwenye Mwezi."

Dkt Schmoll anasema sadfa hii ya matukio matatu ya mwezi kutokea pamoja na jambo la kuwafanya watu kutoka nje na kuutazama.

"Najua watu hawakupenda mwezi huu kuitwa Mwezi Mkubwa, kwani si bayana muonekano wa ukubwa wake ni kiasi gani," anasema Dkt Schmoll.

Mwezi mkubwa unafaa kuonekana ukiwa 7% mkubwa kuliko kawaida na kuangaza mara 15% zaidi ya kawaida.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Urusi, Ulaya, China na India wanapanga kutuma wataalamu kwenye Mwezi (c) SPL

Nchini Kenya, kwa mujibu wa Idara ya Utabiri wa hali ya Hewa, tukio la mwezi kupatwa linafaa kuanza saa 6:57:42 jioni na kumalizika saa 7:08:31 jioni, ingawa mwezi Kenya hautapatwa kikamilifu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii