Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 01.02.2018

Jonny Evans
Image caption Arsenal walitaka kumnunua Jonny Evans

Arsenal walishindwa kumnunua mlinzi wa Ireland Kaskazini Jonny Evans kwa kuchelewa kulipa £12m, huku West Brom pia ikikataa ofa kutoka kwa Manchester City na Everton ya kumchukua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Express and Star)

Mchazaji wa Leicester City Riyad Mahrez, mwenye umri wa miaka 26, ana "masikitiko" kwamba pendekezo la kuhamia Manchester City lilisitishwa na klabu yake, anasema rafiki yake winga huyo wa Algeria. (Sky Sports)

Image caption Lille ilikataa kumuuza Ibrahimu Amadou kwa Crystal Palace

Mshambuliaji wa Leicester City alitoweka kabla ya mchezo wa klabu yake wa Ligi ya Premia ambapo walilazwa 2-1 na Everton Jumatano usiku. (Mirror)

Na Mahrez, mchezaji bora wa mwaka wa 2015-16 chaguo la wachezaji atafanya mazungumzo na meneja wa Leicester Claude Puel baadae wiki hii kuhusu kujumuishwa kwake tena katika kikosi cha Leicester City. (Telegraph)

Crystal Palace ilitangaza kutaka kumnunua kwa hadi £16m beki Mfaransa Ibrahim Amadou lakini klabu ya Lille ikakataa kumuuza kijana huyo mwenye umri wa miaka 24. (Sky Sports)

Image caption Pierre-Emerick Aubameyang anasema alifurahi sana kukutana tena na mchezaji mwenza wa zamani katika timu ya Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan katika Arsenal

Nahodha huyo wa timu ya Lille aliwasili London kujaribu kukamilisha hatua ya kuhamia katika kikosi cha the Eagles. (Croydon Advertiser)

Meneja wa Everton Sam Allardyce anasema kuwa hatima ya wachezaji watano katika kikosi kilichoichapa Leicester 2-1 katika uga wa Goodison Park ilikuwa haijulikani siku ya mwisho ya kipindi cha kuhama wachezaji Jumatano. (Liverpool Echo)

Pierre-Emerick Aubameyang anasema kuwa "ni mwenye furaha sana kujiunga na Miki katika timu" baada ya kukutana tena na mchezaji mwenza wa zamani katika timu ya Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan katika Arsenal, miezi 18 baada ya kucheza pamoja kwa mara ya mwisho. (Daily Mail)

Roma ilisitisha azma yake ya kumtaka mchezaji wa Manchester United Daley Blind baada ya klabu hiyo ya Old Trafford kutaka mkataba wa kudumu kwa ajili ya mlinzi huyo Mholanzi mwenye umri wa miaka 27. (Express)

Image caption Barcelona inammezea mate David Alaba anayeichezea Buyern Munich kwa sasa

Meneja wa Charlton Karl Robinson amekiri kuwa alikuwa tayari kumuuza beki wa kati Ezri Konsa, mwenye umri wa miaka 20, lakini hakuna klabu yoyote miongoni mwa zile zilizomtaka iliyotimiza thamani ya Mwingereza huyo. (South London Press & Mercury)

Barcelona walilenga uhamisho wa mchezaji wa Bayern Munich David Alaba, aliye na umri wa miaka 25.

Imefahamika kuwa Katibu wa masuala ya kiufundi wa klabu hiyo Robert Fernandez alimuomba rais wa klabu Josep Maria Bartomeu kutafuta pesa kwa ajili ya kumnunua mchezaji huyo beki wa kushoto raia wa Austria . (AS)

Rio Ferdinand anadai amedai kuwa alimuona mchezjai mpya wa Tottenham Lucas Moura katika basi ya timu Wembley baada ya winga wa Brazil kukamilisha mpango wake wa kuhamia kaskazini mwa London kutoka Paris St-Germain. (Daily Mail)

Tetesi bora zaidi za Jumatano

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez amefanya mazungumzo na mmiliki Mike Ashley na bado ana ''matumaini'' ya kuwanunua wachezaji zaidi kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kuhama kwa wachezaji . (Mirror)

Lakini Benitez anasisitiza kuwa msimamo wake huenda ukabadilika iwapo juhudi za kuwataka wachezaji kama vile mshambuliaji wa Leicester kutoka Algeria Islam Slimani, mwenye umri wa miaka 29, na mlinzi wa Manchester City Eliaquim Mangala zitafeli. (Northern Echo)

Arsenal watamruhusu bekikutoka Ufaransa Mathieu Debuchy, mwenye umri wa miaka 32, kujiunga na Saint-Etienne kwa uhamisho wa bila malipo. (L'Equipe - Katika Kifaransa)

West Ham wamezungumza na Lille kuhusu kusaini mkataba wa nahodha wao Ibrahim Amadou.

Crystal Palace wamekwisha kamilisha malipo yao kwa ajili ya kumnunua Mfaransa huyo mlinzi mwenye umri wa miaka 24 . (Sky Sports)

Mada zinazohusiana