Iron Biby: Alichekwa kwa kuwa mnene utotoni lakini sasa ni bingwa wa kunyanyua uzani

Cheick Ahmed al-Hassan Sanou Haki miliki ya picha CHEICK SANOU
Image caption Wakati alipotimiza umri wa miaka tisa, Cheick alikuwa amezoea kukejeliwa na kutaniwa

Cheick Ahmed al-Hassan Sanou alikuwa na uzito wa kupindukia kila wakati, lakini hakujua ni kwa kiasi gani ana nguvu mpaka siku ile alipomtupa mmoja watu waliokuwa wakimkejeli hadi upande mwingine wa chumba.

Hii ni habari ya namna kijana aliyezomewa aligeuka na kuwa mshiriki wa mashindano ya mtu mwenye nguvu zaidi duniani.

Ikiwa una miaka 16, na kilo za mwili 122 na kifua upana wa inchi 48 kuna uwezekano mkubwa wa kuonekana mnene zaidi ya wengine na hivyo ndivyo ilikuwa kwa Cheick Ahmed al-Hassan Sanou.

Sanou ambaye alizaliwa Burkina Faso 1992, Biby kama anavyopendwa kuitwa, alitambua kuwa alikuwa tofauti na ndugu zake alipokuwa na umri wa miaka mitano na hilo lilikuwa ni jambo ambalo kidogo lilimtatiza.

"Mama yangu alisema nilikuwa mnene tangu nilipozaliwa- nikiwa na kilo 5 na nilikuwa nikivuta pumzi kwa nguvu -sio kama mtoto mchanga wa kawaida," alitabasamu alipokuwa akielezea maisha yake ya utotoni.

"Nilitaka kuwa mkimbiaji wa mbio fupi maana nilikuwa na kasi ya kukimbia hata kama nilikuwa mzito," aliiambia BBC.

"Lakini kila mara nilipokuwa nikikimbia, mwili wangu ulikuwa unatikisika, na watoto wenzangu shuleni walikuwa wakicheka sana na kuniita 'Fat Boy'. Ilikuwa ni kama burudani kwao, kwa hiyo nikakata tamaa, lakini sikuwahi kuacha nia yangu ya kuwa mwanariadha''.

Kila mara uigizaji na sarakasi pia zilimvutia, lakini kila alipofanya sarakasi yoyote sauti ya mwili wake ukigonga zulia na ilipokelewa na watu kwa kejeli kuashiria kuwa alikuwa hawezi.

Haki miliki ya picha CHEICK SANOU
Image caption "Watu hawakuwa wanene sana nchini Burkina Faso, na wasichana waliokuwa na umri sawa na wangu walipenda vijana wembamba'' alisema

Wakati alipotimiza umri wa miaka tisa, Cheick alikuwa amezoea kukejeliwa na kutaniwa.

Nilijichukia kwa kuwa hivyo - nilikuwa mdogo zaidi katika darasa langu, lakini nilionekana mkubwa kwa miaka minne zaidi ya wenzangu wakiwemo kaka zangu.

"Watu hawakuwa wanene sana nchini Burkina Faso, na wasichana waliokuwa na umri sawa na wangu walipenda vijana wembamba.

Wasichana wakubwa walikuwa wanazungumza nami na kuwa wakarimu, lakini nilipoonyesha aina yoyote ya kutaka urafiki nao walikua wanakataa''

Alivumilia matusi na udhalilishaji bila kukabiliana na yeyote hadi alipofika umri wa kubalehe wakati ambapo aligundua ana nguvu kwa kiwango gani - la kushangaza ilikuwa ni kwa kijana mkubwa ambaye alikuwa akimchokoza.

CHEICK SANOU

Haki miliki ya picha CHEICK SANOU
Image caption Mwaka 2009, Cheik mwenye umri wa miaka 17 alitumwa nchini Canada kukamilisha masomo yake ya sekondari huko alikuwa maarufu kwa kunyanyua uzani wa juu

"Nilikasirika nikasema: 'niache , nikamsukuma mbali, lakini alipaa hadi upande miwingine wa chumba na akashtuka.

Nilishtuka pia, lakini nikajua siku ile kuwa nina nguvu - hakunisumbua tena ."

Wakati mmoja kaka yake alisafiri kwenda Canada mwaka 2007, alimuomba amtumie kifaa cha kukondesha mwili alichokiona kwenye tangazo la kibiashara kwenye jarida lililoahidi wateja kuwa miili yao itakonda.

Lakini kwa kuwa kaka yake hakuweza kupata kifaa hicho alibakia kuwa mnene na mwenye shauku ya kupoteza kilo za mwili.

Kila mbinu aliyoitumia kupunguza uzito wa mwili hakufanikiwa.

Halafu mwaka 2009, Cheik mwenye umri wa miaka 17 alitumwa nchini Canada kukamilisha masomo yake ya sekondari.

Kwenda kwake kulimfanya awe na malengo mapya ya kupoteza uzito . Alijiunga na mazoezi ya mwili (gym) katika siku yake ya kwanza, lakini kitu fulani kilikuwa karibu kutokea ambacho kingemuathiri katika maisha yake yaliyosalia.

Alichaguliwa kama mmoja wa wachezaji wa timu ya kikapu - na kwa mara ya kwanza maishani mwake, alifanya kitu ambacho alikijali sana.

Haki miliki ya picha CHEICK SANOU
Image caption Mwaka 2013, aliingia shindano la kwanza la wanyanyuaji wa uzito mkubwa na akashinda, ukafuatia ushindi katika mashindano ya kitaifa baadaye katika mwaka huo

Kwa kipindi kifupi Cheick alikuwa maarufu katika eneo la kufanyia mazoezi, akinyenyua uzito sawa na wanyanyuaji vyuma wenye taaluma hiyo.

Mnamo mwaka 2013, aliingia shindano la kwanza la wanyanyuaji wa uzito mkubwa na akashinda, ukafuatia ushindi katika mashindano ya kitaifa baadaye katika mwaka huo.

"Kaka yanyu alikua akiniita Iron Biby (Chuma Biby) na jina hili limenifuata kote ninakoenda, lakini nilipoanza kufahamika kwa kunyanyua uzani wa juu nikawa Iron Biby," alikumbuka.

Mashindano ya kimataifa yakafuata kwa hiyo akawa Chuma Biby kweli.

Kwa mtu mgeni, Iron Biby ni mshindani kwani tayari amekwishawapiku watu maarufu kwenye matukio wayapendayo, na hajalenga kukomea hapa.

"Mpango wangu ni kuwa binadamu imara zaidi duniani na kuchukua taji la Burkina Faso," alisema.

Kuonekana kwa udhabiti wake kumewafanya vijana wa Burkina Faso kutamani kuwa kama yeye.

Wengi miongoni mwao ambao walikuwa wakiwatamani kuwa wachezaji soka sasa wanataka kuwa wanaume wenye nguvu(ama wanawake thabiti).