Magufuli ateua Mwanasheria mkuu mpya wa serikali

Rais wa Tanzania John Magufuli Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Tanzania John Magufuli

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Dokta Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali.

Uteuzi huo umeanza jana, Februari mosi.

Kabla ya uteuzi huo Dokta Kilangi, alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughili za mkondo wa juu ya mafuta-PURA.

Wakati huohuo, Rais Magufuli amemteua Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali.

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Paul Ngwembe, Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania.

Kufuatia uteuzi huo, Rais Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa serikali George Mcheche Masaju na Aliyekuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama kuu.

Uteuzi huo pia umeanza jana Februari mosi

Mada zinazohusiana