Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 03.02.2018

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane
Image caption Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Harry Kane

Tottenham imejiandaa kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane 24 kwa Real Madrid iwapo timu hiyo hataipatia presha na kwamba watalipwa dau la £176m. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mkufunzi wa zamani wa Everton na Southampton Ronald Koeman atatangazwa kuwa kocha mpya wa Uholanzi Ijumaa ijayo. Koeman mwnye umri wa miaka 54 amekuwa bila kazi tangu alipofutwa kazi na Everton mnamo mwezi Oktoba. (De Telegraaf - in Dutch)

Image caption David De Gea

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho atamuuza kipa wa Uhispania David De Gea, 27, kwa Real Madrid iwapo kiungo wa kati wa Wales Gareth Bale, 28, atakubali kujiunga na Manchester United (Daily Express via Diario Gol)

De Gea ni mmoja wa walinda lango wanne wanaosakwa na Real Madrid. Kipa wa Chelsea 25, raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois, yule wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak, 25, na kipa wa AC Milan 18, na Italy Gianluigi Donnarumma wanaonekana kuwa mbadala wa David De Gea. (Goal.com)

Image caption Diego Simeone

Mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone hataki kuwa mkufunzi wa Chelsea kwa sababu anataka kukamilisha kandarasi yake ya miaka miwili na nusu iliosalia ijapokuwa angependelea ombi kutoka kwa Manchester United. (Times - subscription required)

Mkufunzi wa Wigan Paul Cook amefanya mzaha kwamba aliificha simu ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Nick Powel katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.

Mchezaji huo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa ananyatiwa na klabu ya Brighton. (Wigan Today)

Image caption Mesut Ozil

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kwamba kumzuia Mesut Ozil na mashaara wa £350,000 kwa wiki ndio lililokuwa chaguo la rahisi la klabu hiyo. (Telegraph)

Wenger pia amesema kuwa alifanya makosa kutomuuza Alexis Sanchez kwa dau la £60m kwa Manchester City mwisho wa msimu uliopita huku akisema kuwa raia huyo wa Chile ameandikisha mkataba ulio na zaidi ya thamani ya £600,000 kwa wiki katika klabu yake mpya. (Mirror)

Mashabiki wa West Ham wanapanga kufanya maandamano dhidi ya mmiliki wa klabu hiyo kabla ya mechi dhidi ya Burnley mwezi ujao. (Sun)

Image caption Kiungo wa kati wa Roma na Ubelgiji Radja Naingolan

Kiungo wa kati wa Roma na Ubelgiji Radja Naingolan mwenye umri wa miaka 29 anasema kuwa atamaliza kipindi chote cha mchezo wake katika klabu hiyo.Anahusishwa na uhamisho wa Chelsea (Sky Sports Italia via Football Italia)

West Brom wamewataka mashabiki wake kuwasili mapema kabla ya mechi dhidi ya Southampton kwa sababu wanataka kumuomboleza Cyrille Regis from 14:00 GMT. (West Brom official website)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Diego Maradona

Mchezaji wa zamani wa Argentina Diego Maradona amenyimwa visa ya kuingia Marekani baada ya kumtusi rais Donald Trump. (Daily Mail)

Mkufunzi wa zamani wa Swansea Paul Clement anasema kuwa uuzaji wa Gylfi Sigurdsson kwa Everton mwisho wa msimu uliopita ulikua makosa na kwamba wachezaji wazuri waliokuwa wakinyatiwa hawakusajiliwa. (Times - subscription required)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amekejeli madai kwamba beki aliyesajiliwa kwa dau la £75m Virgil van Dijk, 26, ni mzito. (Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Virgil van Dijk

Mshambuliaji wa West Ham Javier Hernandez, 29, anasema kuwa alitaka kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari kwa sababu alitaka kushirikishwa zaidi katika mechi.(Mirror)

Kiungo wa kati wa West Ham Michail Antonio, 27, anasema kuwa meneja David Moyes alifanya uamuzi wa sawa wa kumwacha nje baada ya kuchelewa katika mkutano wa timu , akisema kuwa alienda katika eneo ambalo kocha wa zamani Slevn Bilic alikuwa akifanya mikutano yake badala ya uwanja wa klabu hiyo. (Sun)

Mada zinazohusiana