Raheem Sterling: Timu pinzani zinatuchezea rafu

Pep Guardiola alidai kwamba wachezaji wake wanafaa kulindwa sana na marefa. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pep Guardiola alidai kwamba wachezaji wake wanafaa kulindwa sana na marefa.

Winga Raheem Sterling amedai kwamba wachezaji wa Manchester City twamekuwa wakichezewa vibaya na timu pinzani.

Matamshi yake yanajiri baada kocha Pep Guardiola aliyedai kwamba wachezaji wake wanafaa kulindwa sana na marefa.

Ngware waliochezewa wachezaji Brahim Diaz na Kevin de Bruyne wakati wa mechi ya ushindi wa 3-0 dhidi ya West Brom ilimkasirisha Guardiola.Sterling alisema: makabiliano mengine ni mabaya , sio kitu nilichotarajia katika ligi kubwa hususan wakati ambapo timu yako inapoteza unaanza kuwachezea visivyo wachezaji wenzako.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliongezea: Kutakuwa na makabiliano ambayo sio mazuri na pengine hayakuwa ya makusudi.

Lakini wakati huohuo kama rafu mbaya ni rafu mbaya na nadhani marefa na maafisa wanahitaji kupounguza makabiliano kama hayo kwa sababu wachezaji wengine wanapata majeraha mabaya.

Mchezaji huyo wa Uingereza pia anahofia kwamba mojawapo ya makabiliano kama hayo yanaweza kumfanya mchezaji kutoshiriki katika dimba la dunia la 2018 nchini Urusi.

Mada zinazohusiana