Uturuki yapata pigo kubwa vitani Syria

Uturuki imesema kuwa imewatuma wanajeshi zaidi hadi Afrin ili kuwafurusha wanamgambo wa Kikurdi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uturuki imesema kuwa imewatuma wanajeshi zaidi hadi Afrin ili kuwafurusha wanamgambo wa Kikurdi

Jeshi la Uturuki, limepata pigo baya mno vitani, katika makabiliano yake dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi ndani ya Syria Kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya wanajeshi wake 7 kuuwauwa.

Wanajeshi watano waliuwawa, baada ya kifaru chao kushambuliwa katika eneo la Afrin.

Waziri mkuu Binali Yildirim, ameapa kuwa wanamgambo hao "watalipia uovu wao maradufu".

Mara tu baada ya matamshi hayo kutoka Ankara, ndege za kijeshi ziliangusha mizinga mizito mizito kulenga ngome za Wakurdi Kaskazini Mashariki mwa mji wa Afrin.

Operesheni ya Uturuki iitwayo "Olive Branch" ilizinduliwa Januari 20, ili kuwafurusha wanamgambo wa kikurdi wa YPG kutoka maeneo ya Afrin.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji wa kundi la waasi la Free Syrian Army wanapigana kwa pamoja na jeshi la Uturuki

Katika taarifa kutoka idara ya jeshi la Uturuki, wapiganaji wa YPG walishambulia kwa makombora kifaru moja ya jeshi lake katika eneo la Sheikh Haruz, Kaskazini Mashariki mwa mji wa Afrin.

Image caption Ramani

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii