Kylie Jenner ajifungua mtoto wa kike

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Siku ya Jumapili Kylie Jenner alitangaza kuwa amejifungua mtoto wa kike

Nyota nchini Marekani Kylie Jenner amethibitisha Jumpaili kuwa amejifungua mtoto wa kike.

Kumekuwa na uvumi kwamba Kylie mwenye umri wa miaka 20 ni mja mzito, lakini alinyamaa kimya kuhusu uja uzito wake muda wote huu.

Jenner alitangaza katika mtandao wake wa Instagram Jumapili kwamba alijifungua mnamo February mosi. Aliomba radhi kwa ukimya wake na kuwaweka kizani mashabiki zake.

Mtoto huyo ni wa kwanza wa Jenner na mpenzi wake Travis Scott ambaye ni rapa mashuhuri Marekani, na bado mpaka sasa hawajaamua kumpa jina gani.

Kylie Jenner, ambaye ni mtoto wa mwisho katika familia ya Kardashian na Jenner, alipata umaarufu kupitia kipindi cha televisheni 'Keeping Up with the Kardashians', pamoja na dada zake Kendall Jenner, Kourtney, Kim, na Khloé Kardashian.

Yeye ni binti wa mwanariadha wa olimpiki Caitlyn Jenner na nyota mashuhuri wa Televisheni Kris Jenner.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii