Polisi wamkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Mowzey Radio

Mwanamuziki wa Uganda Moses Ssekibogo, anayefahamika zaidi kwa jina la Mowzey Radio wa kundi la Goodlyfe Haki miliki ya picha Will Baose
Image caption Mwanamuziki wa Uganda Moses Ssekibogo, anayefahamika zaidi kwa jina la Mowzey Radio wa kundi la Goodlyfe

Polisi nchini Uganda wamemkamata mtuhumiwa anayehusishwa na mauaji ya mwanamuziki maarufu Mowzey Radio, aliyefariki kutokana majeraha aliyoyapata baada ya mzozo uliotokea kwenye kilabu moja ya burudani '' De Bar'', iliyopo katika mji wa Entebbe.

Wakati wa mazishi yake, mama yake Jane Kasumba aliwalaani wauaji wake imeripotiwa katika magazeti ya Daily Monitor.

Amenukuliwa akisema:

Nimeumizwa sana, sana. Lakini kinachoniumiza zaidi ni kwamba sikuwaona waliomuua mwanangu. Ninawalaani waliomuua mwana wangu. "

"Utawala wa hospitali ya Case wanasikitika kutangaza kifo cha Moses Ssekibogo maarufu kama Mowzey Radio leo tarehe 1 Februari 2018 saa kumi na mbili asubuhi," ilisoma sehemu ya taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Case kuhusiana na kifo chake.

Radio, ambaye jina lake halisi Moses Ssekibogo, alifariki kutokana na majeraha yaliyotokana na kupigwa na mlinzi wa kilabu hiyo ya usiku majuma mawili yaliyopita

Daily Monitor inaripoti kuwa polisi wamewakamata mameneja wa kilabu hiyo kwa mahojiano.

Gazeti la serikali, New Vision imeripot kuwa mamlaka imeifunga kilabu hiyo ili kupisha uchunguzi ufanyike.