Sidanta:Muendelezo wa Mazingira kuwa rafiki unakwama

Enviroment
Image caption Mirija ya plastiki hudumika sana kunywea vinywaji

Mmoja wa watengenezaji wakubwa wa mirija ya plasitiki inayotumiwa kunywea vinywaji bwana John Sidanta amesema muendelezo wa mazingira kuwa rafiki unakwama.

John Sidanta, ambae ni mtendaji mkuu wa Primaplast, alisema kuwa anajua ya kwamba kumeongezeka wasiwasi duniani juu ya viwango vya uchafuzi baharini na ardhini sababu ya Plastiki.

Mtendaji huyo ameleza kuwa njia mbadala na za gharama nafuu za kuweka mazingira kuwa rafiki, hazikuwepo na kwa sasa njia nzuri zina gharama mara mia zaidi.

Kampuni ya Primaplast inazalisha zaidi ya mirija milioni 600, kwa mwezi na huuzwa katika masoko ya Tangerang, Indonesia Ulaya na Japan, ambako zinauzwa pamoja na mabango ya juisi, vinywaji vya yoghurt.

Baadhi ya makampuni tayari yameanza mipango ya kupunguza matumizi yao ya mirija ya plastiki.

Image caption John Sidanta mtendaji mkuu wa kampuni ya kutengeneza mirija ya Plastiki

Sehemu maarufu za vinywaji kama JD Wetherspoon na Pizza Express wametangaza mipango ya kuifungua kabisa, wakati makampuni mengine, kama vile All Bar One, wanasema wana mpango wa kupunguza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mirija ya Plastiki.

Mirija inaweza tengenezwa kwa kutumia viazi au nafaka lakini lakini Bw Sidarta alisema imekuwa ghali sana kuweza kumudu kutengeneza bidhaa kutoka na malighafi za nafaka.

Sidarta Anaamini kwamba serikali duniani kote lazima ziamua sheria wazi ya matumizi ya kimataifa ya vifaa vya plastiki katika chakula na vinywaji na bidhaa nyingine za walaji.

"Tunapaswa kuwa na busara sio kusema 'kuacha kutumia bidhaa' bila suluhisho," alisema Bwana Sidarta

Mada zinazohusiana