Zuma aahirisha hotuba ya taifa

Zuma ameendelea kukataa kuachia madaraka Haki miliki ya picha AFP/GETTY
Image caption Zuma ameendelea kukataa kuachia madaraka

Hotuba ya Rais Jacob Zuma iliyokuwa inategemewa sana bungeni Alhamisi wiki hii imeahirishwa, wakati shinikizo likizidi kuongezeka dhidi yake kuachia madaraka.

Spika wa bunge Beleka Mbete alitoa tangazo hilo bila kutoa tarehe mpya ya hotuba hiyo.

Kamati kuu yenye maaumizi makubwa ndani ya chama cha ANC wameitisha mkutano maalumu siku ya kesho, Jumatano.

Bw Zuma amekataa kung'tuka sababu ya tuhuma za ufisadi.

Aliongoza mkutano na baraza la mawaziri leo asubuhi lakini uendelevu wa utawala wake haukuzungumzwa.

Vyama vya upinzani wanataka kura ya kutokuwa na imani naye ipigwe ilikutoa madarakani. Leo shirika la Nelson Mandela pia lilitoa wito ya kumuomba aachie kiti.

Mada zinazohusiana