Kwa Picha: Wacheza dansi wenye ndoto kubwa

Street dancers in Sierra Leone Haki miliki ya picha Olivia Acland

Wacheza dansi nchini Sierra Leone wanasifa mbaya - mara nyingi wanadhaniwa kama wezi na wahalifu. Kundi la wacheza dansi liitwalo 'Roughest Bounds' wanapinga dhana hiyo. Kundi hilo lenye wanachama 12 wana ndoto ya kufika mbali japo wanakabiliwa na changamoto za jamii na fedha.

Slim Haki miliki ya picha Olivia Acland

Slim, mwenye umri wa miaka 17, amekuwa akizicheza tangu alipokuwa na miaka saba

"Nilipoanza kucheza shuleni, niligundua nina kipaji", anasema. " Watu waliniambia ninafanya vizuri na nilisikia furaha nikiwa nacheza na kupigiwa makofi. Nikaamua kuundeleza kipaji changu"

Slim on his mattress Haki miliki ya picha Olivia Acland

Lakini safari haijawa rahisi. Baba yake Slim, alimfukuza nyumbani na kumuambia asingeweza kupata chochote kama mcheza dansi Afrika.

Sasa kundi hilo linakaa pamoja kwenye nyumba ya vyumba viwili inayomilikiwa na meneja wao, Samuel, aliyewagundua wakicheza mitaani mwaka jana na akaamua kusaidia kuendeleza vipaji vyao.

Wanalala kenye magodoro membamba matatu. Baba yake Samuel, amemshinikiza aache kulisaidia kundi hilo na amewaamuru kuhama nyumbani hapo ifikapo wiki ijayo.

Roughest Bounds practice Haki miliki ya picha Olivia Acland
Roughest Bounds practice Haki miliki ya picha Olivia Acland

'Roughest Bounds' wanafanya mazoezi kila siku kuanzia saa nane mchana hadi saa moja jioni, katika mitaa ya nyumbani kwao na kwenye paa la nyumba yao.

People watch the group going through their routine Haki miliki ya picha Olivia Acland
Roughest Bounds practice Haki miliki ya picha Olivia Acland

Kabla ya kutumbuiza hadharani, kundi hilo husali pamoja. Slima anasema ni muhimu kwa kujenga morali.

The group pray before a performance Haki miliki ya picha Olivia Acland
Performing Haki miliki ya picha Olivia Acland

Pesa kidogo wanayopata inatoka katika kucheza kwenye mashindano ya dansi na harusi.

"Mwaka huu tulishinda mashindano matatu" anasema Slim

"Kila shindano tulitoza kati ya dola za kimarekani 13 hadi 39. Tukicheza kwenye harusi wanatupatia marupurupu tu. Hela hizi hazitoshi- tunazitumia kununua mavazi maalum."

Roughest Bounds Crew necklace Haki miliki ya picha Olivia Acland

Kila mjumbe wa kundi anavaa shanga yenye jina lake na vifupi vya'Roughest Bounds Crew'.

Receiving a meal Haki miliki ya picha Olivia Acland

Baadhi ya siku wavulana hao wanaishiwa hela na kukaa bila kula chakula au kula mlo mmoja tu

Slim at school Haki miliki ya picha Olivia Acland

Slim anaenda shuleni asubuhi . "Najua nataka kuwa mcheza dansi lakini kwanza nahitaji kumaliza shule" anasema

Alitakiwa kufanya mitihani ya taifa mwezi Januari.

The group discuss routines Haki miliki ya picha Olivia Acland

Kila jioni, baada ya mazoezi, vijana hao wanakaa pamoja barazani na kujadiliana ratiba yao kwa kazi za maonesho watakazofanya.

Hapa wanaoengelea namna ya kucheza katika maonesho kwenye hoteli moja Freetown - kaulimbui ilikuwa utamaduni wa Sierra Leone.

Slim dancing Haki miliki ya picha Olivia Acland

Slim akionesha uwezo wake.

Anasema anandoto kubwa ya kudensi Marekani na Ulaya kuonesha watu kwamba "tunavipaji pia hapa Sierra Leone"

Picha zote zilipigwa na © Olivia Acland