Trump aiambia Pentagon iandae gwaride la jeshi Washington

Donald Trump Haki miliki ya picha Getty Images

Rais wa Marekani Donald Trump anaripotiwa kuwauliza maafisa wakuu wa jeshi kuandaa gwaride kubwa zaidi nchini humo kuonyesha nguvu zake za kijeshi.

Afisa anayehusika na masuala ya habari katika ikulu ya white house, Sarah Sanders amesema rais Trump amewaagiza wakuu wa jeshi kupanga hafla hiyo ambayo raia wa taifa hilo watatoa shukrani na heshima zao kwa wanajeshi wao.

Ripoti zinasema kuwa rais Trump alifurahishwa mno na sherehe za Bastille nchini Ufaransa, ambako mbali na wanajeshi kuonyesha wanajeshi wake, magari ya kivita na vifaru pia inajumuisha maonyesho ya ndege za wana anga.

Sasa rais Trump anataka Marekani kuiga mfano huo wa Ufaransa.

Sherehe ambayo anasema itafana zaidi kuliko ya Ufaransa.

Kufuatia agizo hilo maafisa wakuu wa idara ya ulinzi nchini Marekani kwa sasa wanatafakari pendekezo hilo.

Suala muhimu ni tarehe ya sherehe hizo.

Siku ya kuwakumbuka wakongwe wa kivita huadhimishwa tarehe kumi na moja Novemba kila mwaka na inasemekana huenda sherehe hizo zikaandaliwa siku hiyo.

Tayari maeneo matatu ambayo huenda yakafikiriwa kuandaa sherehe hizo yametolewa.

Rais Trump anasemekana kupendekeza sherehe hizo kuandaliwa katika barabara ya Pennsylvania inayoliunganisha bunge la congress na ikulu ya white house na hoteli ya Trump International.

Haki miliki ya picha Reuters

Lakini kuna wasi wasi kuwa baada ya sherehe hizo bara bara hiyo huenda ikaharibiwa kabisa kutokana na uzito wa vifaa vya kijeshi.

Tamasha za kijeshi sio za kawaida nchini Marekani kwa sababu ni ghali.

Sherehe za mwisho za kijeshi kuandaliwa baada ya vita vya ghuba iligharimu serikali dola milioni kumi.

Je ni kila mtu ana ridhia pendekezo hilo?

Wanasiasa wa chama cha Democratic wameshutumu mpango huo kwa gharama kubwa na kusema kuwa fikra hizo zinatoa ishara za kutia wasiwasi.

"Ni njia ovyo ya kupoteza fedha!" alituma ujumbe wa twitter mwakilishi Jim McGovern. "Trump anaonekana kuwa dikteta zaidi ya rais , Wamarekani wanastahili kiongozi bora zaidi."

Mwakilishi Jackie Speier, ambaye ni mwanachama wa kamati ya bunge kuhusu huduma za kijeshi ameliambia shirika la utangazaji CNN: "Nilishangazwa na pendekezo hilo kwa kweli .... tuna kiongozi anayetaka kuwa kama Napoleon."

"It's really a waste of money, and I think everyone should be offended by his need to always be showy... it's not our style, it's not the way we do business."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii