Ni namna gani komando Yosso walizimwa Tanzania?
Huwezi kusikiliza tena

Dr Jaka Mgwabi alifanikiwa kuwazima Komando Yosso nchini Tanzania.

Kuzuka kwa makundi ya uhalifu katika nchi za Afrika na Ulaya si jambo jipya.Tanzania husasan katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini humo wanalikumbuka vyema kundi la Komando Yosso ambalo lilikuwa tishio na linalotajwa kuwa baya kuwahi kutokea.

Dr Jaka Mgwabi Mwambi aliyehudumu katika nyadhifa mbali mbali serikalini, wakati huo akiwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es alifanikiwa kuwazima Komando Yosso.

Mwandishi wa BBC Leonard Mubali,amfanya mahojiano na Dr Jaka Mwambi,ambaye kwanza anaanza kuwaelezea komando Yosso.

Mada zinazohusiana