Jaji mkuu wa Kenya amewataka wanasiasa kutii sheria

Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga

Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha sheria na katiba ya kenya katika kukabiliana na upinzani .

Tamko hilo limekuja mara tu baada ya kiongozi mmoja wa upinzani wakili Miguna Miguna kufukuziwa nchini Canada,baada ya kuzuiliwa na polisi kwa siku tano hata baada ya mahakama kutoa amri kwamba aachiliwe kwa dhamana .

Katika maelezo yake jaji David Maraga ,amesema malalamiko yaliyopelewekwa mahakamani yalikuwa wazi ,na yalikuwa majukumu ya mahakama kufanya maamuzi kwa kuwa ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe.

Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama.

Licha ya kuwa serikali ya Kenya kupitia wizara ya mambo ya ndani kujitetea kwa ufafanuzi juu ya uraia wa wakili huyo wa upinzani Miguna Miguna,kwa msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka kusema kwamba kiongozi huyo "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wa nchi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009,wakati ambao uraia wa nchi mbili ulikuwa hauruhusiwi .

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii