Tangazo bandia la kifo cha mfadhili wa upinzani Kenya lazua hisia

Notisi iliondikwa na gazeti la nation likiomba msamaha kufuatia kisa hicho
Image caption Notisi iliondikwa na gazeti la nation likiomba msamaha kufuatia kisa hicho

Gazeti moja nchini Kenya limeomba msamaha kwa kuchapisha tangazo la mazishi ya mfadhili maarufu wa muungano wa upinzani nchini humo licha ya kuwa hai.

Gazeti la Daily Nation lilisema kuwa limechapisha tangazo la ''kifo'' cha Jimi Wanjigi kimakosa na kwamba lilikuwa linashirikiana na maafisa wa polisi kubaini aliyechapisha tangazo hilo.

Makundi ya haki za kibinaadamu yamesema kuwa tangazo hilo ni sawa na kutoa vitisho vya mauaji.

Mfanyibiashara Wanjigi alifadhili kampeni ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga ya uchaguzi uliopita.

Washirika kadhaa wa bwana Odinga wamekamatwa na kupewa vitisho.

Mada zinazohusiana