Mwanamke adai mumewe alimuibia figo ili kujilipa mahari India

Mwathiriwa anasema kuwa figo yake ilitolewa bila yayeye kujua. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwathiriwa anasema kuwa figo yake ilitolewa bila yayeye kujua.

Mwanamke mmoja nchini India amedai kuwa mumewe na nduguye wa kambo wamekamatwa baada ya kuambiwa maafisa wa polisi walimuibia figo moja ili kujilipia mahari.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba mumewe mwanamke huyo kutoka Magharibi mwa Bengal alipanga upasuaji wa eneo moja la matumbo yake wakati alipokuwa akiugua uchungu katika tumbo lake.

Baadaye mwaka 2017, alifanyiwa vipimo viwili vya ukaguzi wa kimatibabu ambavyo vilibani kwamba figo yake moja haipo.

Anadai kwamba mumewe mara kwa mara alitaka kulipwa mahari yake .

Malipo ya mahari hiyo ambayo hulipwa familia ya mume kutoka kwa familia ya mke nchini India yamepigwa marufuku nchini India tangu 1961.

Akizungumza na vyombo vya habari nchini India, mwathiriwa Rita Sarkar , alisema amekuwa mwathiriwa wa mgogoro wa kinyumbani kutokana na mahari hiyo kwa miaka mingi.

''Mumewe wangu alinipeleka katika hospitali ya kibinfasi mjini Kolkata, ambapo yeye na maafisa wa matibabu waliniambia kwamba atapona atakapotolewa eneo hilo la utumbo lililovimba kupitia upasuaji'' , gazeti la Hindustan lilimnukuu akisema.

''Mumewe wangu alinionya kutozungumza kuhusu upasuaji huo kwa mtu yeyote mjini Kolkata''

Huwezi kusikiliza tena
Kijiji ambacho wanawake 'huwabeba wanaume' Rwanda

Miezi kadhaa baadaye mwanamke huyo alikuwa akihisi vibaya na akapelekwa hospitalini na watu wa familia yake.

Uchunguzi ulibaini kwamba figo yake ya upande wa kulia ilikuwa imetolewa, alisema.

Ukaguzi wa pili wa kimatibabu ulithibitisha ukweli huo.

''Baadaye nilijiuliza ni kwa nini mume wangu alinitaka kunyamazia upasuaji niliofanyiwa', aliambia gazeti la Hindustan Times.

''Aliuza figo yangu kwa sababu familia yangu haikuweza kumlipa mahari yake''.Mwanamke mmoja nchini India amedai kuwa mumewe na nduguye wa kambo wamekamatwa baada ya kuambiwa maafisa wa polisi walimuibia figo moja ili kujilipia mahari.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii