Kilimo cha teknolojia kisichohitaji mtandao

Kilimo cha teknolojia kisichohitaji mtandao

Takriban wakulima nusu milioni katika maeneo ya mashambani barani afrika na amerika kusini wanapeana mawaidha wakitumia teknolojia ambayo haihitaji wao kuwa na mtandao.

Teknolojia ya wefarm imewawezesha wakulima kujadiliana kupitia ujumbe mfupi wanayoiandika kwa lugha wanayoielewa, ambayo hutafsiriwa ili wakulima wengine waweze kuielewa na kupeana ushauri wao.

Mwandishi wa BBC Judith Wambare alikutana na wakulima nchini Kenya ambao walimueleza kwa kina jinsi teknlojia hii inavyowasaidia.