Afrika Kushiriki michezo ya majira ya baridi Pyeongchang

afrika

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nchi nane kutoka Afrika kushiriki michuano ya Afrika

Nchi nane za kiafrika zinashiriki katika michuano ya mwaka huu ya Olimpiki ya majira ya baridi huko Pyeongchang ,Korea kusini.

Bara la Afrika ambapo ni mojawapo ya mabara yaliyo na joto zaidi, halina michezo ya msimu wa baridi kama vile kuteleza kwenye theluji.

Lakini licha ya kuwa na changamoto hiyo ,washiriki ambao wako kwenye viwango vya juu wanatoka barani Afrika katika nchi za Nigeria,Eritria,Ghana,Madagasca,Afrika kusini,Morocco na Togo watashiriki katika michuano hiyo ya Pyeongchang.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sabrina Simader kutoka Kenya ni mshiriki wa michezo ya majira ya baridi

Sabrina Simader kutoka Kenya ni mshiriki mwenye umri wa miaka 19 na anasema anafurahia sana kucheza michezo .

Simader, ambaye familia yake ilihamia Austria wakati akiwa na miaka mitatu, na anakuwa mtelezaji wa kwanza wa kwenye milima kuiwakilisha Kenya kwenye michuano ya olimpiki ya majira ya baridi

Alikuwa mtelezaji mshindani kwenye mchezo huu mwaka 2013 na mwaka 2016 aliziwakilisha nchi za afrika mashariki kwenye michuano kama hii ya majira baridi nchini Norway .

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Michuano ya Olimpiki majira ya baridi

Wakati,Akwasi Frimpong anasema kuwa huwa inachukua karibu miaka minne mpaka sita kuweza kuwa bora na imara kushindana sababu mchezo una kwenda haraka sana kiasi kwamba akili yako haiwezi hata kushikato

Akwasi Frimpong alianzisha shirikisho la taifa la Bobsled na Skeleton (BSF-Ghana) mwaka 2016.

Aidha licha ya kuwa michuano hiyo kuwa ni faraja kubwa kwa wanamichezo hao kutoka Afrika lakini pii ushiriki wao ni historia kwa nchi za Kiafrika kushiriki katika michuano hiyo kwa nchi kama Nigeria na Eritrea.