Maafisa wa Uganda wapata kashfa ya wakimbizi

sudan

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wakimbizi wengi nchini Uganda wametoka Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Sudani Kusini

Maafisa wanne wa Uganda wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kupungua kwa idadi ya wakimbizi nchini Uganda.

Apollo Kazungu ambaye ni mkuu wa kusimamia wakimbizi nchini humo pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu wanafanyiwa uchunguzi pia juu ya suala hiyo.

Aidha uchunguzi huo utaweza kubaini kama maafisa wa umoja wa mataifa walikuwa wanahusika pia.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Uganda ina wakimbizi milion 1.4

Hata hivyo Uganda inatajwa kupokea wakimbizi million 1.4 na hivyo kupelekea kukaribisha wakimbizi idadi kubwa zaidi ya nchi nyingine yeyote kwa mwaka 2016 na wengi wakiwa wametoka Sudan Kusini na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo(DRC)

Lakini inawezekana tuhuma hizo zisiwe za kweli kutokana na namba ya wakimbizi .Mpaka sasa ,Uganda imesifiwa sana kwa sera zake za kuwakaribisha wahamiaji na kutajwa kuwa ni miongoni mwa maeneo yanayochukua idai kubwa ya wakimbizi duniani.

Hivyo majibu ya uchunguzi unaofanywa ndio utaeleza ukweli ya mambo na hatua ambazo zitachukuliwa.