Tetesi za soka Ulaya Jumapili 11.02.2018

Antonio Conte

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Antonio Conte

Kipa wa England na Stoke Jack Butland, 24, anawinda na Liverpool na Arsenal wa kima cha paunia milioni 40. (Sun on Sunday)

Chelsea wanataka meneja Antonio Conte kuondoka klabu hiyo msimu wa joto wakati wa kumalizika mkataba wake, badala ya kumfuta kazi sasa. (Sunday Telegraph)

Everton wanamlenga meneja wa Shakhtar Donetsk kuchukua wajibu wa meneja wa sasa Sam Allardyce msimu wa joto. (Mail on Sunday)

Manchester City wamekubali mkataba wa pauni milioni 50, kumsaini kiungo wa kati raia wa Brazil Fred kutoka Shakhtar Donetsk 24, msimu ujao. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kevin de Bruyne

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 26, ambaye yuko kwenye mkataka huko Manchester City hadi mwaka 2023, atakamilisha taaluma yake akicheza katika ligi kuu kwa mujibu wa ajenti wake. (Sun on Sunday)

Liverpool wameanza kummezea mate wing'a wa Bayer Leverkusen' raia wa Jamaica Leon Bailey. (Sunday People)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewambia Real Real Madrid kuwa kipa wa Uhispania David de Gea, 27, haondoki klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Roberto Firmino

Mshambuliaji raia wa Brazil Roberto Firmino, 26, anasema huenda akasalia katika klabu ya Liverpool kwa muda mrefu. (Esporte - in

Tottenham wana uhakika kuwa Mauricio Pochettino atabaki kuwa meneja wao licha ya Real Madrid kummezea mate. (Sunday People)

Mshambuliaji raia wa Algeria Islam Slimani, 29, anatajia kuindoka Leicester kwenda Newcastle kwa mkataba wa kudumu. (Leicester Mercury)