Miji 11 iliyo kwenye hatari ya kukumbwa na ukosefu wa maji ya kunywa kama Cape Town

Dripping tap

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Robo ya miji yote duniani hukumbwa na changamoto za maji

Cape Town uko katika hali mbaya ya kuwa mji wa kwanza katika yakati hizi kuishiwa na maji ya kunywa.

Hata hivyo hali inayounumba mji huo wa Afrika Kusini ni mfano wa tatizo ambalo wataalamu wamekuwa wakionya kwa miaka kuhusu uhaba wa maji.

Licha wa kuchukua asilimia 70 ya dunia, maji hasa maji ya kunywa ni haba, ni asilimia 3 tu ya maji hayo yanaweza kuwa salama kwa kunywa.

Zaidi ya watu bilioni moja hawana maji na wengie bilini 2.7 hukumbwa na uhaba wa maji kwa takriban mwezi mzima kwa mwaka

Kwa hivyo hapa kuna miji mingine 11 ambaye inaweza kukumbwa na ukosefu wa maji duniani.

1. São Paulo

Mji wa kibiashara wa Brazil na moja ya miji 10 yenye watu wengi zaidi duniani ulikubwa na hali sawa na iliyoukumba mji wa Cape Town mwaka 2015.

Wakati huo mji huo wa wakaazi milioni 21.7 ulikuwa na chini ya siku 20 za kuwa na maji na polisi walilazimika kuyalinda magari yenye maji kuzuia uporaji.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ukame uliokumwa mji wa sao paulo

Ilifikiriwa kuwa ukame ulioathiria maeneo ya Kusini na masharikia mwa Brazil kati ya mwaka 2014 na 2017 ulisabaisha lakini ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sao Paulo ulilaumu mamlaks kwa kuwa na mipangilio duni na uwekezaji mdogo.

2. Bangalore

Maafisa katika mji huo ulio kusini mwa India wameshangazwa na kuundelea kukua kwa miundo msingi na majengo mapya hasa kutokana na mji wa Bangalore kuzidi kukuwa kama kituo cha kiteknolojia na kushindwa kusimamia ipasavyo vituo ya maji na maji taka.

Sawa na China, India inakumbwa na changamoto na uchafuzi wa maji na Bangalore sio tofauti, Uchunguzi umebaini kuwa maziwa asilimia 85, yana maji yanayoweza kutumiwa kwa kilimo na viwandani.

Hakuna hata ziwa moja lililo na maji safi ya kunywa na kuoga

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Uchafuzi wa maji maziwa wa Bangalore

3. Beijing

Benki ya dunia inaroddhsha kukosa maji wakati watu walio eneo fulani hupata chini ya cubic mita 1,000 za maji safi kwa kila mtu.

China ina asilimia 20 ya watu wote duniani lakini ina asilimia 7 tu ya maji safi ya kunywa.

4. Cairo

Mto muhimu nchini Misiri, Mto Nike uliokuwa na umuhimu mkubwa, umekumbwa na matatizo mengi nyakati hizi.

Huchangia asilimia 97 ya maji yote nchini Misri lakini pia maji machafu kutoka kwa kilimo na kutokana shughuli za binadamu huishia hapo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nile huchangia asilimiA 97 ya maji nchini Misri

UmojA wa mataifa unakadiria kuwa huenda kukawa uhaba mkubwa wa maji mwaka 2025.

5. Jakarta

Sawa na miji mingi iliyo pwania, mji huu mkuu wa Indonesia unakumbwa na tatizo la kupanda kwa bahari.

Kufuatia sababu kuwa chini ya nusu ya watu milioni 10 wana maji ya mfereji, kuna uchimbaji haramu wa visima, hatua hiyo inakausha maji yaliyo ardhini.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mafuriko Jakarta

6. Moscow

Urusi ina kiwango kikubwa cha majia safi ya kunywa lakini uchafuzi uliosababishwa na viwanda ni tatizo kubwa.

Inaaminiwa kuwa asilimia kati 35 na 60 ya maji ya kunywa nchini Urusi hayatimizi viwango vinavyohitajika.

7. Istanbul

Kulingana na tarakimu za serikali ya Uturuki, nchi sasa kwa inakubwa na tatizo kubwa la maji.

Waatalamu wanaonya kuwa hali itakuwa mbaya zaid ifikapo mwaka 2030.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Ukame wa miezi 10 ulikausha ziwa hili karibu na Istanbul

Miaka ya hivi karibuni maeneo yaliyo na watu wengi kama mji wa Istanbul yanaendelea kukumbwa na uhaba wa maji nyakati kuna ukosefu wa mvua.

8. Mexico City

Ukosefu wa maji sio jambo geni kwa wakaazi milioni 21 katika mji huo mkuu wa Mexico.

Mmoja kati ya watu watano hupata saa chae za maji kutoka kwa mifereji yao kila wiki.

9. London

Kati ya miji yote duniani, London sio mji wa kwanza unaoingia akilini wakati wa kufikiria suala la uhaba wa maji.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Asilimia 25 ya maji hutumiwa vibaya London

Lakini kwa mujibu wa mamlaka ya mji huo, mji huo unazidi kukubwa na matatizo ya kujipata kwrnyr shidaa ifikapo 2021 na matatatizo mabaya ifikapo 2040.

10. Tokyo

Ukiwa nyumbani kwa watu milioni 30, Tokyo una mifumo ya maji inayotengea maji yaliyo juu ya ardhi yaani mito, maziwa na barafi inayoyeyuka.

11. Miami

Jimbo la Florida nchini Marekani ni kati ya majimbo matano yanayopokea mvua kila mwaka, hata hivyo kuna janga katika mji maarufu wa jimbo hilo, Miami.

Mapema karne ya 20 mradi wa kukausha eneo lenya unyevunyevu ulisababisha kitu fulani. Maji yenye chumvi kutoka kwa bahari ya Atlantic yalichafua chanzo kikuu cha maji safi ya mji huo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Uchaguzi unaotokana na maji ya bahari