Ndege yenye abiria 71 yaanguka ikipaa nchini Urusi

Ndege iliyotoweka ya An-148 ni sawa na iliyo kwenyr picha hii

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Ndege iliyotoweka ya An-148 ni sawa na iliyo kwenyr picha hii

Ndege ya Urusi iliyokuwa imebeba abiria 71 na mhudumu imeanguka baada ya kupoteza mawasiliano ilipokuwa ikiondoka uwanja wa mjini Moscow.

Ndege hiyo ya shirika la Saratov ya An-148, ilikuwa safarini kwenda mji wa Orsk wakati ilipoteza mawasiliano.

Huduma za dharura ziliambia vyombo vya habari kuwa ndege hiyo ilianguka na hakuna uwezekano wa kuwapata manusura,

Inaripotiwa kuanguka karibu na Argunovo kilomita 80 kusini mashariki mwa Moscow.

Kulingana na shirika lingine na habari ndege hiyo ilipotea kutoka mitambo ya rada dakika mbili baada ya kuondoka uwanja wa Domodedovo.

Mabaki ya ndege hiyo na miili ilipatikana imetapakaa eneo kubwa. Kifaa kimoja cha kurekodi safari za ndege kimepatikana.

Rais Vladimir Putin ametuma rambi rambi zake kwa familia za waathiriwa na kutaka uchunguzi kufaywa kuhusu kilochosabaisha ajali hiyo.