Hoteli ya kifahari walimozuiwa wanawafalme nchini Saudi Arabia imefunguliwa

The Ritz Carlton in Riyadh on 11 Feb

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha,

Zaidi wa wanawafalme 200, mawaziri na wafanyabiashra wamekuwa wakizuiliwa kwenye hoteli hii na hoteli zingine.,

Hoteli ya kifahari ambayo ilitumiwa kama gereza la kuwashikilia wanawafalme kadhaa na maafisa wengine wa vyeo vya juu katika oparesheni ya kupambana na ufisadi imefunguliwa.

Wahudumu wa hoteli ya Ritz-Carlton iliyo mjini Riyadh waliiambai BBC kuwa hoteli hiyo ilikuwa ikiwachukua wageni,.

Zaidi wa wanawafalme 200, mawaziri na wafanyabiashra wamekuwa wakizuiliwa kwenye hoteli hiyo na hoteli zingine.,

Mwishoni mwa mwezi Januari mkuu wa mashtaka nchini Saudi Arabia alisema kuwa dola bilioni 100 zilikuwa zimekusanywa.

Hii ni kufuatia makubaliano yaliyoafikiwa na wale waliokuwa wamezuiliwa.

Ofisi ya mkuu wa mashtaka ilisema kuwa watu 56 bado walikuwa wanazuiliwa, licha ya baadhi ya ripoti kusema kuwa wale wale waliosalia walikuwa wametolewa hotelini na kupelekwa gerezani.

Kati ya wale walioachiliwa ni mwanamfalme na mfanyabiashara bilionea Alwaleed bin Talal.

Mkuu wa ulinzi Miteb bin Abdullah, ambaye wakati mmoja alionekana na mrithi wa ufalme aliachiliwa mwezi Novemba baada ya kukubalina na mamlaka katika maafikiano yaliyogharimu zaidi ya dola bilioni moja.

Mtoto huyo wa mflame wa zamani wa miaka 65 alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa kuzuiliwa.