Mwanariadha mzaliwa wa Kenya anayetaka kuiwakilisha Somalia michezoni

Mwanariadha mzaliwa wa Kenya anayetaka kuiwakilisha Somalia michezoni

Mwanariadha mzaliwa wa Kenya kutoka Garissa, Abdirizak Abdirahman, anataka kuiga mfano wa mwenzake Mohamed Daud wa Wajir aliyeamua kuikimbilia Somalia michezo ya Olimpiki ya Rio huko Brazil mwalka 2016. Tayari Abdirahman ameanza mpango wa kubadilisha uraia wake akimbilie Somalia, akisema amechoshwa na hali ilivyo kwa sasa anakotoka. Abdirahman ni miongoni mwa wakimbiaji sita wa Garissa walioshiriki mashindano ya kitaifa ya mbio za nyika mjini Nairobi jana. Hamna mmoja wao aliyemaliza katika nafasi kumi bora. Hivyo basi walirudi nyumbani vichwa chini kwani hawakuweza kupata nafasi katika timu ya wanariadha 24 waliochaguliwa kuiwakilisha Kenya kwenye mbio za nyika za Afrika mwezi ujao nchini Algeria. Amezungumza na John Nene.