Wachunguzi wasaka mabaki ya ndege iliyoanguka Urusi

Chanzo cha picha, VASILY MAXIMOV/ GETTY
Mwanaume akionesha sehemu ya ndege iliyopatikana katika eneo ambappo ndege iliodondoka
Wachunguzi nchini Urusi wanaendelea kusaka maeneo yaliofunikwa na theluji karibu na jiji la Moscow ilikupata fununu za kwanini ndege hiyo ilidondoka
Sikua ya Jumamosi, ndege ya Urusi iliyokuwa imebeba abiria 71 na wahudumu ilianguka baada ya kupoteza mawasiliano ilipokuwa ikiondoka uwanja wa ndege mjini Moscow.
Maafisa wanasema sababu zinapelekea kuwa hali ya hewa, hitilafu za kibinadamu na kiteknolojia.
Tukio hili halijahusishwa kwa namna yoyote na ugaidi. Ndege hiyo ilikuwa inaelekea Orsk kwenye milima ya Ural.
Ilianguka karibu na kijiji cha Argunovo, kilomita 80 kusini mashariki ya Moscow. Mabaki ya ndege na miili ilisambaratika katika eneo hilo.
Chanzo cha picha, DMITRY SEREBRYAKOV/GETTY
Waokoaji na wachunguzi wakichambua mabaki ya ndege
Mtoto na vijana wawili walikuwa miongoni mwa miili ya abiria iliyo patikana, kwa mujibu wa chombo cha habari cha Tass.
Waokoaji walilazimika kuacha magari yao na kutembea kwa mguu hadi eneo ambalo ndege iliangukia.
Msemaji wa idara ya uchunguzi Svetlana Petrenko, amesema kuwa operesheni hiyo ya kusaka eneo hilo itachukua siku moja kwa mujibu wa mtandao wa habari wa The Gazeta.ru
Ndege hiyo haikupiga simu ya dharura lakini rikoda moja imepatikana.
Chanzo cha picha, Flighradar24
The Flightradar24 website shows the flight path
Rais Vladimir Putin ametoa salaam za rambirambi kwa familia za waathirika. Nchi za Marekani na Uingereza zote zimesema kuwa "wamehuzunika sana" na tukio hilo.
Hii ni mara ya kwanza ndege ya abiria inaanguka katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja- mwaka 2017 ilikuwa mwaka wa usalama zaidi katika rekodi ya usafiri wa anga.
Ndege yenye abiria 71 yaanguka ikipaa nchini Urusi
Kulingana na shirika lingine na habari ndege hiyo ilipotea kutoka mitambo ya rada dakika mbili baada ya kuondoka uwanja wa Domodedovo.