Marekani: Tuko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini

Dada yake Kim Jong-un, Kim Yo-jong aliketi nyuma ya makamu wa rais wa Marekani Mike Pence Haki miliki ya picha AFP/Getty images
Image caption Dada yake Kim Jong-un, Kim Yo-jong aliketi nyuma ya makamu wa rais wa Marekani Mike Pence

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amesema kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini bila ya kuwepo masharti yoyote.

Katika kile kinachoonekana kama kubadilska kwa mnsimamo wa Marekani, Bw Pence aliliambia gazeti la the Washington Post kuwa ikiwa Korea Kaskazini inataka mazungumzo, basi utawala wa Trump utafanya hivyo.

Lakini amesisitiza kuwa vikwazo vitakuwepo hadi Korea Kaskazini ichukue hatua za kumaliza mpango wake wa silaha za nyuklia.

Bw Pence alikuwa akizungumza akiwa njiani kutoka kwa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi nchini Korea Kusini, ambapo alifanya mazungumzo na Rais Moon Jae-in.

Utawala wa Trump awali ulisema kuwa hautafanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jon-un ikiwa tu yuko tayari kuachana na mpango wa nyuklia.

Mada zinazohusiana