Gatdet Dak afungwa Sudan Kusini

Haki miliki ya picha Atlas
Image caption Ramani ya Sudan kusini

Msemaji wa zamani wa kundi la waasi wa Sudan kusini amehukumiwa adhabu ya kifo baada ya kukutwa na hatia ya uhaini.

James Gatdet Dak, ambaye alikuwa akifanya kazi na Riek Machar, Makamu wa Rais wa zamani nchini humo, aliyeamua kuchukua silaha na kupambana na Rais Salva Kiir kwa zaidi ya miaka minne iliyopita.

Gatdet alisafiri nchini Kenya mwaka 2015 na kupewa hadhi ya ukimbizi.

Hata hivyo alirudishwa nchini mwake Sudan kusini baada ya kuonesha kwake kuunga mkono uamuzi wa Umoja wa Mataifa wa kumfukuza Mlinda amani mwandamizi raia wa Kenya.

Kurudishwa nchini mwake kulilaaniwa na mashirika ya haki za binadamu.

Mada zinazohusiana