Kim Jong-un aishukuru Korea Kusini kwa makaribisho mema

Photo of the North Korean delegation and Mr Kim
Maelezo ya picha,

Picha ya KCNA ikionyesha Kim Jong-un, akiwa na Bi Kim Yo-jong (kushoto) na Kim Yong-nam (kulia)

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameisifu Korea Kusini kwa jitihada zake nzuri za kuukaribisha ujumbe kutoka Kaskazini wakati wa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi.

Matamshi yake yanakuja huku ujumbe, ulioongozwa na dada yake Kim Yo-jong uliporejea nyumbani kutoka Pyeongchang.

Shirika la habari la serikali KCNA lilisema kuwa Bw Kim aliishukuru Korea Kusini kwa kuupigia debe uwepo wake katika mbio hizo.

Kuhudhhuria kwa Korea Kaskazini kumekuwa kwa mchango mkubwa kwa uhusiani kati ya nchi hizo.

Lakini kumekuwa pia na wasi wasi kuwa hiyo imeruhusu Korea Kaskazini kufanikiwa katika propaganda zake.

Bi Kim na mkuu wa nchi asiye na madarakani Kim Yong-nam waliakuwa miongoni mwa maafisa wakuu waliokuwa kwenye ujumbe wa Korea Kaskazini kuzuru Korea Kusini tangu vita vya Korea Kaskazini miaka ya 1950.

Sikua ya Jumamosi Kim alimualika rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, kuzuru Pyongyang kwa mazungumzo. Ikiwa mkutano huo utafanyika utakuw wa kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja kati ya viongozi wa Korea mbili.

Mwaliko huo unakuja hukua uhusino kati ya Korea zote ukionekana kuboreka.