Mke wa Trump Jr apelekwa hospitalini baada ya kufungua bahasha yenye unga

The couple have five children together
Maelezo ya picha,

Trump Jr na Vanessa wana watoto watano

Mke wa mtoto wa Rais Trump, Trump Jr, Vanessa Trump, amepelekwa hospitalini kama njia ya kuchukua tahadhari baada ya kufungua bahasha yenye unga mweupe.

Barua hiyo ilikuwa imetumwa kwa Donald Trump Jr, mtoto wa kwanza wa kiume wa Rais Trump, katika nyumba yake huko Manhattan.

Bi Trump na watu wengine waiokuwa neo hilo waliondolewa na wazima moto na kisha kupelekwa hospitalini.

Polisi wa mjini New York waliiambia BBC kuwa waliifanyia uchunguzi unga huo na kupata kuwa haukuwa na madhara.

Walisema kuwa Bi Trump hakuonekana kuthiriwa na unga huo.

Bw Trump baadaye aliandika katika mtandao wa Twitter na kukashifu kitendo hicho.

Maelezo ya picha,

Familia ya Trump

Kulingana na kituo cha CBS mjini New York mama yake Vanessa Trump, alishika barua hiyo kabla ya Vanessa kuifungua.

Walinzi wa rais wanasema wanaichunguza barua hiyo.

Donald Trump Jr ambaye anafanya biashara ya baba yake, alimuoa née Vanessa Kay Haydon Novemba mwaka 2005 katika eneo la starehe la Trump huko Forida.

Shangazi ya Trump Jr, jaji Maryanne Trump Barry, alisimamia sherehe hiyo

Kabla ya kuolewa na Trump Jr, Vanessa alikuwa mwanamitindo huko New Nork.