Karani adai nyoka alikula mamilioni ya pesa Nigeria

Python Haki miliki ya picha SPL
Image caption Karani adai nyoka alikula dola 100,000 Nigeria

Karani mmoja nchini Nigeria amefukuzwa kazi baada ya kuwaambia wakaguzi wa hesabu kuwa nyoka alikula naira milioni 36.

Pesa hizo ni sawa na dola 100,000 za kimarekani.

Karani Philomena Chieshe alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya bodi ya mtihani ya Nigeria inayokusanya pesa za mtihani.

Bodi hiyo ya mtihania iliiambia BBC kuwa ilitupilia mbali madai yake na imeanisha kumchukulia hatua za kinidhamu.,

Kisa hicho kimezua shutuma na dhihaka kwenye mitandao ya kijamio nchini Nigeria.

Nayo tume ya kupambana na rushwa nchini Nigeria iliandika ujumbe huu katika Twitter ambayo nembo yake ni mwewe.

Mada zinazohusiana