Aina mpya ya antibiotic yagunduliwa katika mchanga

bakteria ndani ya mchanga Haki miliki ya picha Science Photo Library

Wanasayansi nchini Marekani wamegundua aina mpya ya dawa aian ya antibiotic katika sampuli za mchanga.

Viini hivyo asilia huenda vinaweza kutumika kukabiliana na maambukizi, kikundi cha wataalamu wa chuo kikuu cha Rockefeller kinatumai.

Utafiti unaonyesha kuwa viini hivyo vinavyojulikana kama malacidins, vinaangamiza kikamilifu magonjwa kadhaa yanayoambukizwa na bakteria yanayokaidi aina nyingi zilizopo za antibiotic ikwemo MRSA.

Wataalamu wanasema utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Microbiology, linatoa matumaini mapya katika jitihada za kuunda dawa hizo.

Magonjwa yanayokaidi madawa ndio tishio kubwa katika afya duniani.

Husababisha vfo vya watu 700,000 kwa mwaka, na dawa mpya zinahitajika kwa dharura.

Dawa kutoka kwenye uchafu.

Mchanga umejaa mamilioni ya viini vinavyoweza kuchangia kuundwa mchanganyiko unaotibu, zikiwemo antibiotic.

Kundi la Dkt Sean Bradykatika chuo kikuu cha Rockefeller mjini New York limekuwa na shughuli kubwa kuchunguza viini hivyo.

Walitumia mfumo wa ukaguzi wa jini kukagua zaidi ya sampuli 1000 zilizokuanywa kutoka maeneo tofuati Marekani.

Walipogundua malacidin katika sampuli nyingi, walihisi kwamba huu ni ugunduzi muhimu.

Walifanya majaribio ya walichokusanya kwa kuwapa panya waliokuwa na vidonda na ilisaidia kuondosha maambukizi hayo kwenye vidonda mwilini.

Watafiti hao sasa wanajitahidi kuimarisha makali ya daw ahiyo kwa matarajio kwamba itaweza kutengenezwa kuwa dawa ya tiba kwa magonjwa ya binaadamu.

Dkt Brady amesema: "Ni vigumu kusema nilini au hata iwapo ugunduzi wa viini vya aina hii vya malacidin vinaweza kuishia katika zahanati.

"Ni hatua ndefu kutokea ugunduzi wa uwepo wa antibiotic hadi kuundwa kuwa dawa ya kutumika katika taasisi za afya."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii