Mipango ya siri ya kuurithi uongozi wa Jumuiya ya madola

Malkia akiwa katika shule ya msingi ya Mayflower Primary School huko Poplar, Londona mashariki 2017 Haki miliki ya picha PA

Jumuiya ya madola imeanza kufikiria kwa siri ni nani atakayemrith Malkia kama kiongozi, BBC imegundua.

Suala hilo ni zito kwasababu wadhifa huo sio wa kurithi na hautokwenda moja kwa moja kwa mwanamfalme wa Wales atakapofariki malkia.

Jumuiya hiyo imeunda 'kundi la kiwango cha juu' kutathmini jinsi jumuiya hiyo ya kimataifa inavyoongozwa.

Kundi hili linakutana baadaye rasmi kukagua namna jumuiya ya madola inavyoendeshwa na afisi kuu na magavana waliopo.

Limesema suala kuhusu urithi wa uongozi wa jumuiya sio sehemu ya jukumu la kundi hilo, lakini imetajwa kwamba mazungumzo ya siku nzima ni ya 'wazi'.

Hatahivyo, duru za kiwango cha juu zimeongeza kuwa mkutano wa kundi hilo London utatafakari ni nini kitakachofanyika wakati Malkia anayetimia miaka 92 mwezi Aprili atakapofariki.

Mmoja alisema: "Natarajia suala la urithi litazuka, licha ya kuwa sio jambo litaloonekana kwa uzuri."

Ajenda ya mkutano kama ilivyoonekana na BBC inasema kutakuwa na majadiliano 'yatakayotafakari utawala mpana', ambayo duru za ndani zinasema ni ujumbe was siri wa suala la urithi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Malkia akiwapongeza washindi wa tuzo ya Jumuiya ya madola kwa vijana 2016

Malkia alitangazwa kuwa kiongozi wa jumuiya ya madola katika kutawazwa kwake mnamo 1953, alipokuwa kiongozi wa taifa wa matifa 7 kati ya nane wanachama.

Licha ya kwamba Malkia alirithi uongozi huo kutoka kwa Mfalme George VI, sio wadhifa wa kurithi utakaomwendea moja kwa moja mwanawe - atakaye kuwa kiongozi mkuu wa mataifa 15 kati ya 53 yaliomo katika jumuiya hiyo ya madola.

Ni nini Jumuiya ya madola?

  • Ni muungano wa mataifa yliokuwa chini ya utawala wa kikoloni wa Uingereza, na mataifa mengine pia.
  • Ilianzishwa mnamo 1931
  • Kuna mataifa wanachama 53
  • Makao yake makuu yapo London
  • Takriban watu bilioni 2.4 wanaishi katika mataifa ya jumuiya ya madola
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Inadhaniwa kuwa mwanamfalme Charles ndiye atakayemrithi Malkia kama kiongozi wa jumuiya madola

Uamuzi wowote kuhusu mustakabali inabidi uchukuliwe na viongozi wa serikali wanachama katika Jumuiya hiyo wakatiwa kifo cha Malkia. Lakini hakuna mfumo rasmi wa kumchagua mrithi wake.

Licha ya kwamba wengi katika Jumuiya hiyo wanachukulia hakuna mrithi mwingine zaidi ya Mwanamfalme Charles, katika siku za nyuma kumekuwa na mazungumzo kuhusu kumchagua kiongozi kuimarisha hadhi ya kidemokrasi ya jumuiya hiyo.

Kundi hilo la kiwango cha juu, linalojumuisha mawaziri wa ngazi ya juu wa zamani kutoka jumuiya hiyo, watakutana katika makao makuu ya jumuiya hiyo London katika jumba la Marlborough.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii