Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atishia kuishambulia Syria

French President Emmanuel Macron Haki miliki ya picha AFP
Image caption Akiongea mjini Paris siku ya Jumanne Macron alielezea msimamo wake kuwa matumizi ya silaha za kemikali ni kuvuka mstari mwekundu wa serikali yake.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametishia kuishambulia Syria ikiwa ushahidi utaibuka kuwa serikali ya Syria inatumia silaha za kemikali dhidi ya raia.

"Tutashambulia maeneo ambapo silaha hizi hutengezwa au penye mipango hii hufanyiwa," aliwaambia waandishi wa habari.

Lakini Bw Macron alisema kuwa uchunguzi bado haujaonyesha kuwa silaha zilizoharamishwa zimetumiwa.

Matamshi yake yanafuatia ripoti kadhaa za mashambulizi ya kutumia silaha za Chlorine nchini Syria tangu mwezi Januari.

Watu tisa walitibiwa kwa matatizo ya kupumua baada ya bomu linaloaminwa kujazwa na kemikali kuangushwa katika mji unaoshikiliwa na waasi mapema mwezi huu.

Upinzani nchini Syria ulisema kuwa helikopta ya serikali iliangusha bomu eneo la Saraqeb katika mkoa ulio kaskazini mashariki wa Idlib.

Serikali ya Syria inakana kutumia silaha za kemikali na kusema kuwa haiwalengi raia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Matamshi yake yanafuatia ripoti kadhaa za mashambulizi ya kutumia silaha za Chlorine nchini Syria tangu mwezi Januari.

Akiongea mjini Paris siku ya Jumanne Macron alielezea msimamo wake kuwa matumizi ya silaha za kemikali ni kuvuka mstari mwekundu wa serikali yake.

"Leo hii mashiria yetu, vikosi vyetu havijathibitisha kuwa silaha za kemikali zimetumiwa dhidi ya raia," alisema.

"Mara hilo linatakapothibitishwa kuwa kweli, nitatenda kile nilisema. Lengo ni kuwapiga vita magaidi."

Mwaka uliopita Bw Macron alimuambia raia wa Urusi Vladimir Putin kuwa matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria itakuwa ni kuvuka mstari mwekundu hali ambayo itachangia hatua kutoka Ufaransa.

Katika mazungumzo kwa njia ya simu na Putin siku ya Ijumaa, Bw Macron alilezea wasi wasi kuhusu dalili zinazoonyesha kutumika kwa Chlorine dhidi ya raia wiki za hivi karibuni, kwa mujibu wa ofisi yake.

Mada zinazohusiana