Mfungwa ambaye alitumia ndugu yake pacha kutoroka jela Peru amekamatwa

Alexander Delgado in a police car in custody
Maelezo ya picha,

Akiongea na vyombo vya habari Alaxander Delgadoi alisema alitotoroka kwa sababu alikuwa ana hamu sana ya kumuona mama yake.

Mamlaka nchini Peru zimemkamata mfungwa zaidi ya mwaka mmoja tangu atoroke jela kwa kumuacha ndugu yake pacha katika nafasi yake

Alexander Delgado alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 16 wa dhuluma ya kingono kwa mtoto na wizi kwenye gereza moja kaskazini mwa Lima.

Wakati ndugu yake pacha alimtembela gerezani mwezi Januari mwaka uliopita, Alexander alimwekea dawa ya kulevya, akambadilisha nguo zake na kutoroka jela.

Mabadiliko hayo kwa wafungwa yalithibitiswa wakati alama za vidole za Giancarlo zilichukuliwa.

Baada ya miezi 13 mafichoni Alexander Delgado alaikamatwa siku ya Jumatatu katika mji wa bandari wa Callao baada ya wizara ya masuala ya ndani kutangaza zwadi kuhusu bahari ambazo zingepelekea akamatwe.

Sasa anatarajiwa kuhamishwa kwenda kwa grereza lenye ulinzi mkali kusini mwa nchi.

Wakati Alexander akiwa mafichoni ndugu yake Giancarlo alikamatwa na kuchunguzwa akishukiwa kushirikiana na pacha wake.

Lakini hakushtakiwa na sasa ameachiliwa.

Akiongea na vyombo vya habari Alaxander Delgadoi alisema alitotoroka kwa sababu alikuwa ana hamu sana ya kumuona mama yake.