Je gharama ya uzazi katika baadhi ya mataifa Afrika mashariki ikoje?

Wakunga nchini Uganda huwazalisha kati ya akina mama 350 hadi 500 kwa mwaka. Haki miliki ya picha Gus Gregory
Image caption Wakunga nchini Uganda huwazalisha kati ya akina mama 350 hadi 500 kwa mwaka.

Mama ameelezea furaha yake baada ya zahanati moja ya kibinfasi nchini Gabon kumuachilia mtoto wake mchanga miezi mitano baada ya kuzaliwa kutokana na kakosa kulipwa bili ya hospitali.

Mama yake mtoto Angel ameiambia BBC kuwa maziwa yake yamekauka baada ya kutenganishwa na mtoto wake kwa muda wa miezi mitano.

Pia alilalamika kuwa mtoto huyo hajapewa chanjo yoyote.

Kisa hicho kiliishangaza nchi na baadaye akapata msaada kutoka kwa umma.

Image caption Angel ameruhusiwa kurudi nyumbani kwa mamake na familia yake

Bili ya dola 3,630 ililipwa baada ya kampeni kuanzishwa kwa niaba ya familia.

Rais Ali Bongo alikuwa miongoni mwa wale waliotoa mchango wao.

Mkurugenzi wa kliniki hiyo alikamatwa Jumatatu kwa mashtaka ya kumteka nyara mtoto, lakini mashtaka hayo yakaondolewa baadaye.

Je gharama ya uzazi katika baadhi ya mataifa Afrika mashariki ikoje?

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, takriban wanawake 830 hufariki kutokana na sababu zinazoweza kuepukika zinazohusiana na uja uzito na kujifungua ikiwemo gharama za kupokea hudumu za afya.

99% ya vifo hivyo vyote hutokea katika mataifa yanayoendelea. Je hali iko vipi kwa baadhi ya maatifa ya Afrika mashariki?

Kenya:

Kenya imekuwa ikishuhudia kiwango kikubwa cha vifo vya akina mama waja wazito. Kutokana na hilo serikali iliidhinisha sera ya utoaji huduma za bure kwa kina mama wanaojifungua katika taasisi za umma tagu Juni 2013.

Sera hii imekuwa ikiwawezesha wanawake waja wazito kupata huduma za bure wakati wa kujifungua katika vituo vya afya vya umma.

Mpango uliopo ni kwamba vituo hivyo vya afya hutoa huduma ya bure na baadaye serikali inavilipa kupitia wizara ya afya kulingana na idadi ya akina mama waliozalishwa.

Huwezi kusikiliza tena
Wanaume wafungwa uzazi kwa pamoja Kenya

Pia hakuna malipo yanayotolewa kwa huduma za kabla na baada ya kujifungua kwa akina mama na watoto kwa hadi wiki sita.

Licha ya huduma hiyo ya bure,kiwango cha hudumu zinazotolewa bado kinazusha maswali mengi huku baadhi ya wazazi katika hospitali hizo za umma wakiishia kujifungua katika hali duni na wengine hata kuishia kulala kitanda kimoja na wazazi wenzao.

Sio wengi wanaoweza kumudu gharama za hospitali za kibinafsi nchini.

Uganda:

Suala moja kubwa linalohusiana na afya ya uzazi ni nafasi ya akina mama kufikia huduma za dharura na za kiwango bora za uzazi na changamoto nyinginezo kwa wanawake nchini Uganda kufikia huduma hizi, zikiwemo gharama kubwa. Kama nchi nyingine nyingi zinazoendelea, Uganda inashuhudia kiwango kikubwa cha akina mama wanaofariki wakati wa kujifungua - jambo linalodhihirisha ufikiwaji wa huduma hizo za afya.

Hata wakati huduma hizo zinapatikana, kwa kawaida idadi ya wahudumu, dawa na vifaa hospitalini inakuwa ndogo ikilinganishwana idadi ya akina mama wanaohitaji hudumu hiyo.

Muongozo uliotolewa na shirika la Afya duniani ni kwamba mkunga mmoja anastahili kuwazalisha takriban wanawake 175 kwa mwaka, lakini wakunga nchini Uganda huwazalisha kati ya akina mama 350 hadi 500 kwa mwaka.

Upungufu na usambazaji mbovu wa wahudumu wa afya unaathiri kwa jumla gharama ya huduma ya afya ya uzazi na watoto.

Tanzania:

Idadi ya wanawake wanaofariki wakati wa uja uzito na kujifungua nchini Tanzania, kati ya 454 kwa kila visa 100,000 vya kujifungua - ni miongoni mwa zilizo kubwa duniani.

Licha ya kwamba serikali imeahidi kuisaidia hali, idadi hiyo ya vifo haijapungua.

Huwezi kusikiliza tena
Kituo kinachowapa tabasamu wanaougua fistula Tanzania

Na zaidi ya asilimia 70 ya idadi jumla ya raia nchini wanaoishi katika maeneo ya mashamabani ambako wanatatizo kufikia huduma za afya.

Kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya magonjwa katika maeno ya joto na afya ya umma kutoka chuo kikuu cha Heidelberg, Ujerumani kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Muhimbili, kwa jumla wazazi wanaopokea huduma hizo hugharamia malazi, madawa pamoja na usafiri.

Haki miliki ya picha WATERAID/ELIZA DEACON
Image caption Zaidi ya 70% ya raia Tanzania wanaoishi katika maeneo ya mashambani wana tatizo kufikia huduma za afya

Na usafiri hugharimu nusu ya kiwango jumla cha gharama nzima. Malipo yasiyo rasmi hayajumuishwi katika hesabu, na gharama nzima hutegemea huduma inayotolewa kutoka taasisi hata taasisi.

DRC:

Licha ya ufadhili wa kimataifa, kiwango cha huduma za uzazi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imezongwa na miongo kadhaa ya vita vya kiraia nchini pamoja na kudorora kwa hali za kijamii na kiuchumi na miundo mbinu duni.

Kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni ya serikali, takriba 40% ya akina mama waliojifungua Kinshasa hawakujifungua katika hospitali za umma hali inayoashiria kuwa kiwango fulani walipokea huduam hizo katikataasisi zisizo chini ya wizara ya afya nchini.

Miongoni mwa mambo yanayozingatiwa na mzazi kabla ya kutafuta huduma za uzazi asilimia 21 wanasema wamezingatia gharama za huduma hizo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii