Korea kusini yatoa fedha kwa kaskazini

Michezo ya Olympic, Korea kusini
Image caption Michezo ya Olympic, Korea kusini

Maafisa wa Korea kusini wamesema serikali ya nchi hiyo iliidhinisha matumizi ya dola za kimarekani zaidi ya milioni mbili na nusu kwa ushiriki wa Korea kaskazini katika michezo ya Olympic ya majira ya baridi iliyokuwa ikifanyika katika mji wa PyeongChang.

Fedha hizo zilitoka katika bajeti ya Ushirikiano wa Korea, italipia gharama zikiwemo za usafiri, malazi na chakula ya zaidi ya washiriki mia nne na washangiliaji wao.

Kamati ya kimataifa ya Olympic, itaangalia gharamaza wanariadha wa Korea kusini.

Waziri wa Korea kusini Cho Myoung-gyon ameelezea ushiriki wa Korea kaskazini katika mashindano hayo kama tukio muhimu la kihistoria ambalo linafungua milango katika kupata amani katika Rasi ya Korea.

Mada zinazohusiana