Ukame Cape Town umekuwa 'Janga la kitaifa'

Mabwawa ya Cape Town kwa sasa yana asilimia 24.9 pekee ya maji Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabwawa ya Cape Town kwa sasa yana asilimia 24.9 pekee ya maji

Afrika kusini imetangaza ukame unaoshuhudiwa Cape Town - mji unao elekea kuishia bila ya hata tone la maji - kuwa janga la kitaifa.

Serikali ilitoa tangazo hilo baada ya kukagua upya ukubwa na athari ya ukame huop wa miaka mitatu.

Umeathiri vibaya majimbo matatu ya majimbo tisa nchini humo.

Uamuzi huo umejiri wakati Cape Town umetangaza kuwa hatua za kupunguza matumizi ya maji, zinazohitaji kila raia asitumie zaidi ya lita 50 za maji kwa siku - imesaidia kuisogeza mbele "Day Zero" siku ambayo mji utakuwa hauna hata tone la maji hadi Juni 4.

Ni wiki chache tu zilizopita tarehe iliyotolewa wakati mabomba yalitarajiwa kukauka Cape Town ilikuwa ni Aprili 12.

Mmusi Maimane, kiongozi wa chama cha Democratic Alliance (DA), kinachosimamia miji ya Cape Town na jimbo la Western Cape province, alisema katika ujumbe wake wa Twitter:

Kiwango cha maji yanayotumika kwa wastani katika mji wa Cape Town, mji ulio na takriban watu milioni 4, ni chini ya lita milioni 550. Miaka miwili iliyopita ilikuwa ni zaidi ya lita bilioni kwa siku.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watu wamelazimika kuunda foleni kuchota maji kujaliza akiba yao katika mji wa Cape Town

Limekuwa jukumu gumu kwa wakaazi wa mji huo wa Cape Town. Kima walichopewa cha lita 50 za maji kwa siku hutoshi kuoga kwa dakika chache tu na kuvuta maji chooni mtu anapokwenda haja huku mahitaji mengine kama kufua nguo mara moja kwa iki yakizangatiwa pia.

Hatahivyo uamuzi wa kutangaza janga la kitaifa unamaanisha kuwa serikali kuu - inayodhibitiwa na chama tawala ANC - sasa itawajibika katika jitihada za kutoa usaidizi.

Kwa mujibu wa mtandao ya wa shirika la habari eNCA, waziri wa ushirikiano nchini Des van Rooyen wiki iliopita alisema zaidi ya dola milioni 5.8 zimetengwa kukabiliana na janga hilo katika jimbo la Cape ya Magharibi, pamoja na ya Mashariki na Kaskazini, majimbo mawili ambayo hayajaangaziwa vilivyo kwenye vyombo vya habari lakini ambayo pia yanakabiliwa na athari za ukame.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii