Kenya yashushwa uwezo wake wa kukopa
Huwezi kusikiliza tena

Kenya yashushwa uwezo wake wa kukopa kimataifa. Ina maana gani kwako?

Kenya imeshushwa kwenye orodha ya viwango vya uwezo wa kukopa na shirika la kukadiria uwezo wa mataifa kuchukua mikopo - Moody. Sababu kubwa inayotajwa kuchangia kushukishwa kutoka kiwango cha B1 hadi B2 - ni mikopo mingi inayochukua serikali ya Kenya ndani na hata nje ya nchi dhidi ya pato jumla la nchi.

Kwa sasa Kenya iko zaidi ya viwango kumi chini ya Marekani inayoonekana kuwa na uchumi thabiti katika kiwango cha AAA - ambacho ndicho kiwango bora zaidi cha uwezo wa taifa lolote kuchukuwa mikopo.

Je kushushwa kwa kiwango cha Kenya ina maana gani kwa mwananchi? Msikilize hapa mwanauchumi nchini Kenya Paul Wafula:

Mada zinazohusiana