Wakili wa Trump akiri kumlipa 'kisiri' nyota wa filamu za ngono

Wakili wa kibinafsi wa muda mrefu wa rais wa Marekani Donald Trump amekiri kibinafsi kumlipa nyota wa filamu za ngono $130,000 (£95,000) mwaka 2016, Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wakili wa kibinafsi wa muda mrefu wa rais wa Marekani Donald Trump amekiri kibinafsi kumlipa nyota wa filamu za ngono $130,000 (£95,000) mwaka 2016,

Wakili wa kibinafsi wa muda mrefu wa rais wa Marekani Donald Trump amekiri kibinafsi kumlipa nyota wa filamu za ngono $130,000 (£95,000) mwaka 2016, katika taarifa kwa vyombo vya habari vya Marekani.

Hatua hiyo inajiri ripoti ya vyombo vya habari kwamba nyota huyo wa filamu za ngono kwa jina Stromy Daniels alilipwa katika makubaliano ya kutozungumzia uhusiano fulani.

Kwanza alisema kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na rais Donald Trump mwaka 2011 katika mahojiano.

Wakili huyo awali alikuwa amesema kuwa bwana Trump alikataa kuwepo kwa uhusiano wowote kati yao.

Malipo hayo hayakutolewa na shirika la Trump wala kampeni ya bwana Trump.

Anasema aliiambia hivyo hivyo tume ya uchaguzi baada ya kundi moja kuwasilisha malalamishi kuhusu malipo hayo likidai kwamba ulikuwa mchango wa kampeni ya Trump.

''Malipo hayo yaliofanywa kwa bi Clifford yalikuwa halali na haukuwa mchango wa kampeni kutoka kwa mtu yeyote'', alisema.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Trump na nyotawa filamu za ngono Stormy Daniels kulia

Katika mahojiano ya 2011 na jarida la InTouch magazine, nyota huyo wa ngono anasema kuwa alianza uhusiano na rais Trump 2006 baada ya Melania Trump kujifungua mwanawe Barron.

Ripoti hizo zilizuka mwezi Januari wakati jarida la Wall Street liliporipoti kwamba alilipwa ili kuficha makubaliano fulani karibu na uchaguzi wa 2016 hatua iliomzuia kuzungumzia madai hayo.

Bi Clifford aliaminika kujadiliana na vyombo vya habari vya Marekani kuhusu kuhusu swala hilo katika chombo kimoja cha runinga, ripoti hiyo ilisema.

Akijibu maswali kutoka CNN kuhusu ni kwa nini malipo hayo yalifanywa, bwana Cohen alisema: kwa sababu sio ukweli haimanishi kwamba itakuathiri ama kukuharibia.

''Nitamtetea Trump kila siku''.alisema.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii